Pata taarifa kuu
zimbabwe

WikiLeaks yazungumzia afya ya Mugabe, Mfalme Mswati azidi kupingwa

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anasumbuliwa na saratani ya tezi la kibofu ambalo linaweza kusababisha kifo chake kufikia mwaka elfu mbili na kumi na tatu nyaraka za siri za Marekani zilizovijishwa na Mtandao wa WikiLeaks zimeweka bayana.

Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema mnamo mwaka elfu mbili na nane ndipo Rais Mugabe alipogunduliwa kuwa na maradhi hayo na madakatari wakaweka bayana atakuwa na uwezo wa kuishi si zaidi ya miaka mitano.

Mtandao wa WikiLeaks umemnukuu Gavava wa Benki ya Zimbabwe Gideon Gono mwaka elfu mbili na nane mwezi Juni wakati akimwambia balozi wa Marekani hali ya afya ya Rais huyo aliyekaa madarakani tangu uhuru wa nchi hiyo.

Wakati huohuo Wananchi wa Swaziland wanaingia katika siku yao ya pili ya maandamano ya amani yatakayodumu kwa juma moja kushinikiza serikali nchini humo kukubali kuruhusu mfumo wa vyama vingi pamoja na kutafuta suluhu ya mgogoro wa bajeti ya nchi hiyo.

Waandamanaji wapato mia tano walianza maandamano yao hapo jana kwenye Mji Mkuu Mbabane wakiimba na kucheza katika mitaa mbalimbali ikiwa ni ishara ya kutuma ujumbe kwa utawala wa Mfalme Mswati wa III.

Maandamano haya ambayo yameandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi pia yanalengo la kumtaka Mfalme Mswati wa III kupunguza matumizi ya anasa yanayofanya na wake zake kumi na watatu wanaotumia magari ya kifahari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.