Pata taarifa kuu
Swaziland

Maandamano yaendelea nchini Swaziland kwa siku ya pili

Maelfu ya raia nchini Swaziland wanashiriki katika siku ya pili ya maandamano nchini humo wakionesha kuchukizwa kwao na na namna rais wa Taifa hilo anavyoshughulikia matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Reuters/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya waandamanaji elfu tatu wameandamana nchi nzima hii leo wakisindikizwa na askari wa usalama.

Waandamanaji wanashutumu serikali yao kwa ukosefu wa huduma za afya madhubuti na uchumi unaoporomoka,huku makundi ya waathirika wa virusi vya ukimwi wakilalamikia ukosefu wa dawa za kutosha za kurefusha maisha.

Zaidi ya asilimia 25 ya raia wa swaziland wenye umri wa kati ya miaka kumi na mitano na arobaini na tisa wanaaminika kuwa na virusi vya ukimwi nchini humo.

Mazungumzo ya vyama vya wafanyakazi yamegonga mwamba wiki hii baada ya wanachama kupandwa ghadhabu wakimshutumu mfalme wa nchi hiyo Mswati wa 3 kwa matumizi mabaya ya fedha ya uma.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.