Pata taarifa kuu
RIADHA-PARIS

Paul Lonyangata na mkewe Purity watawala mbio za Paris Marathon

Wanariadha kutoka nchini Kenya Paul Lonyangata na mkewe Purity Rionoripo ndio mabingwa wa makala ya 41 ya Paris Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Ufaransa.

Purity Rionoripo na Paul Lonyangata, wanariadha wa Kenya walivyoshinda mbio za Paris Marathon Aprili 9 2017
Purity Rionoripo na Paul Lonyangata, wanariadha wa Kenya walivyoshinda mbio za Paris Marathon Aprili 9 2017 Eric FEFERBERG / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lonyangata alimaliza mbio za Kilomita 42 kwa muda wa saa mbili, dakika sita na sekunde 10, akifuatwa na Mkenya mwenzake Stephen Chebogut, aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa saa 2, dakika 6 na sekunde 56.

Mkenya mwingine Solomon Yego, alimaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa saa mbili, dakika saba na sekunde 13.

Rionoripo naye alishinda mbio hizo kwa muda wa dakika saa mbili, dakika 20 na sekunde 55 na kuweka rekodi mpya kwa upande wa wanawake.

Huu ni ushindi wa kihistoria kwa mume na mke kushinda mashindano haya.

Huu ni ushindi mkubwa kwa wakenya baada ya kupokea habari mbaya kutoka kwa Chama cha riadha duniani IAAF, kuwa bingwa wa olimpiki katika mbio hizi mwaka 2016 Jemima Sumgong alitumia dawa iliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.

Mbali na taji la Olimpiki, Sumgong alikuwa anatetea taji la London Marathon ambalo sasa hatakwebda kushiriki tarehe 23 mwezi huu wa Aprili baada ya kubainika kutumia dawa hiyo.

Hata hivyo, IAAF inasubuiriwa kutoa ripoti zaidi kuhusu uchunguzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.