Pata taarifa kuu
EURO 2016 - URUSI

Kinara wa shirikisho la mashabiki Urusi, afukuzwa Ufaransa

Kiongozi mkuu wa shirikisho la mashabiki wa Urusi wenye msimamo mkali, amefukuzwa nchini Ufaransa, kutokana na kujihusisha kwake na kuhamasisha vurugu zilizoshuhudiwa mwishoni mwa juma lililopita mjini Marseille, baada ya mechi ya ufunguzi wa michuano ya kombe la Ulaya 2016, baina ya Urusi na Uingereza.

Sehemu ya mashabiki wa Urusi wanaohudhuria michuano ya kombe la Ulaya 2016, wamekuwa wakikamatwa na maofisa wa Ufaransa na kurejeshwa nchini mwao kwakujihusisha na vurugu
Sehemu ya mashabiki wa Urusi wanaohudhuria michuano ya kombe la Ulaya 2016, wamekuwa wakikamatwa na maofisa wa Ufaransa na kurejeshwa nchini mwao kwakujihusisha na vurugu REUTERS/Benoit Tessier Livepic
Matangazo ya kibiashara

 

Alexander Shprygin ni miongoni mwa mashabiki wengine zaidi ya 20 wa Urusi, wanaosafirishwa kutoka mjini Lille na Marseille na sasa wanarejeshwa kwa nguvu nchini mwao.

Kiongozi huyu na mashabiki wengine, walikamatwa kabla na baada ya mechi ya makundi ya michuano ya kombe la Ulaya baina ya timu yao iliyokuwa inaikabili timu ya taifa ya Slovakia.

Kukamatwa kwa Shprygin, sambamba na mashabiki wengine, kumeikasirisha Serikali ya Urusi, ambayo leo ilimuitisha balozi wa Ufaransa mjini Moscow, kujieleza kutokana na operesheni inayoendelea dhidi ya mashabiki wao.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Urusi, imeeleza kusikitishwa na namna ambavyo vyombo vya usalama nchini Ufaransa vinawafanyia mashabiki wake, na kuonya kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri uhusiano wa nchi hiyo mbili.

Shprygin, na shirikisho lake la mashabiki, anaungwa mkono na utawala wa Kremlin, na ameripotiwa akiandika maandiko ya kibaguzi na yenye msimamo mkali, sawia na kutoa saluti yenye ishara ya wafuasi wa utawala wa kinazi.

Taarifa kutoka shirikisho la mpira la Urusi, imesema kuwa Shprgin na mashabiki wengine wameshapelekwa kwenye kituo maalumu ambako watasafirishwa kurejeshwa nchini mwao, ndani ya siku tano zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.