Pata taarifa kuu
UAE-SYRIA-USHIRIKIANO

UAE yafungua upya ubalozi wake nchini Syria baada ya miaka 7

Nchi ya Falme za Kiarabu imefungua tena ubalozi wake katika mji mkuu wa Syria, Damascus, baada ya kupita zaidi ya miaka saba tangu ulipoanza mgogoro wa ndani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu umefungliwa upya katika mji wa Syria, Damascus, Alhamisi Desemba 27, 2018.
Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu umefungliwa upya katika mji wa Syria, Damascus, Alhamisi Desemba 27, 2018. REUTERS/Omar Sanadiki
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inaonesha kuwa, Syria imeanza kurejeshwa kwenye Umoja wa nchi za Kiarabu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari ya Syria, shughuli za kuufungua upya ubalozi huo wa Imarati mjini Damascus zimefanyika leo Alkhamisi. Ubalozi huo ulifungwa na Abu Dhabi muda mfupi baada ya kuanza mgogoro wa Syria mwaka 2011.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ulianza kuwa mbaya mwaka 2012, baada ya Falme za kiarabu, kuishtumu Syria kwa kukiuka haki za binadamu za raia wake.

Bendera ya taifa hilo imeonekana ikipepea tena katika Ubalozi huo.

Desemba 16, Rais Omar al-Bashir wa Sudan alifanya safari nchini Syria na kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuitembelea nchi hiyo; siku chache baada ya Bunge la Arab League kutaka Syria irejeshwe kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

Nchi ya Falme za Kirabu inafungua upya ubalozi wake nchini Syria siku chache baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuwa majeshi ya nchi hiyo yataondoka katika ardhi ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.