Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-ISRAEL

Kerry awaonya wabunge wa Marekani dhidi ya kuidhinisha vikwazo vipya kwa nchi ya Iran

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry amewaonya wabunge nchini humo kuhusu hatua yao mpya ya kutaka kuidhinisha vikwazo zaidi kwa nchi ya Iran kushinikiza iachane na mpango wake wa Nyuklia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii leo wabunge wa Republicans na wale wa Democrats wanatarajiwa kukutana na kujadili mapendekezo mapya ya vikwazo dhidi ya Iran, jambo ambalo waziri Kerry anaonya kuwa litasababisha vita kwenye eneo la mashariki ya kati.

Waziri Kerry amewaraka wabunge hao kuchana kwanza na mpango wao wa kupitishwa kwa vikwazo zaidi dhidi ya Iran na badala yake wasubiri kwanza maazimio ya mkutano wa Geneva ambao umeelekea kupata muafaka kuhusu mpango wa Nyuklia wa Tehran.

Wabunge nchini Marekani wanaamini kwa sehemu kubwa kuongeza vikwazo zaidi kwa nchi ya Iran kutaifanya iachane na mpango wake wa Nyuklia jambo ambalo linaungwa mkono pia na nchi ya Israel ambayo inataka vikwazo dhidi ya Iran viongezwe.

Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa miezi miwili iliyopita, waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema ili Iran iachane na kurutubisha Nyuklia ni lazima jumuiya ya kimataifa iongeze vikwazo zaidi kwa nchi hiyo.

Nchi ya Marekani inashiriki mazungumzo ya Kampala na ujumbe wa Serikali ya Iran na tayari imeonesha matumaini yake ya kufikiwa kwa mufaka kati ya mataifa ya magharibi na utawala wa Tehran.

Rais wa Marekani Barack Obama ameendelea kusisitiza msimamo wake kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kwamba nchi yake haitakaa kimya na kutazama utawala wa Tehran ukiendelea kurutubisha Nyuklia kwa kutengeneza silaha za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.