Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Odinga: Tume ya Uchaguzi haikutushirikisha kuamua tarehe mpya ya Uchaguzi

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya NASA Raila Odinga amesema Tume ya Uchaguzi haikuwashirikisha kabla ya kutangaza tarehe mpya ya Uchaguzi wa urais ambayo imepangwa kufanyika tarehe 17 mwezi Oktoba.

Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA
Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Odinga amesema uchaguzi huo uliopangwa hautafanyika iwapo mashauriano ya kina hayatafanyika kati ya wahusika wote ili kutatua tofauti mambo yanayozua mvutano ndani ya Tume hiyo.

Pamoja na hilo, Odinga amesema upinzani upo tayari kushiriki katika Uchaguzi huo mpya na kukosoa madai ya chama cha Jubilee kuwa hawataki kushiriki kwenye Uchaguzi huo.

Aidha, kinara huyo wa NASA ametaka Tume ya Uchaguzi kuruhusu wagombea wote walioshiriki katika Uchaguzi uliofutwa mwezi uliopita  kuwania urais.

Hatua hii imekuja baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kuwa wagombea wawili Uhuru Kenyatta na Raila Odinga ndio watakaokuwa katika karatasi ya kupigia kura.

Ekuru Aukot aliyewania urais kupitia chama cha Third Way Alliance, amekwenda katika Mahakama ya Juu kuitaka Tume ya Uchaguzi kuwaruhusu wagombea wengine kushiriki.

Pamoja na hilo, Odinga ametaka kufanyiwa marekebisho ndani ya Tume ya Uchaguzi lakini pia kampuni ya Ufaransa ya Safran kutopewa kazi ya kujumuisha matokeo kieletroniki.

Odinga ameitaka serikali ya Ufaransa kuichunguza na kuifugulia mashtaka kampuni hiyo.

Hata hivyo, chama cha rais Uhuru Kenyatta cha Jubilee kimekuwa kikitaka kutofanyika kwa marekebisho yoyote ndani ya Tume hiyo na Uchaguzi na Uchaguzi mpya kufanyika haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.