Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Mahakama nchini Kenya yasitisha ufungaji wa kambi ya wakimbizi ya Daadad

Mahakama Kuu jijini Nairobi nchini Kenya, imeamua kuwa serikali nchini humo haina mamlaka ya kufunga kambi kubwa ya wakimbizi ya Dadaab.

Kambi ya wakimbizi ya Daadab kaskazini mwa nchi ya Kenya, inayohifadhi wakimbizi wa Somalia
Kambi ya wakimbizi ya Daadab kaskazini mwa nchi ya Kenya, inayohifadhi wakimbizi wa Somalia UNHCR - kenya
Matangazo ya kibiashara

Jaji John Mativo amesema kuwa uamuzi wa serikali ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo kwa sababu wananchi hawakuhusishwa kikamilifu.

Uamuzi huu ni habari njema sana kwa maelfu wa wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi katika kambi hiyo kubwa duniani.

Kabla ya uamuzi huu, wakimbizi walikuwa na hofu ya kurudi nyumbani kwa kuhofia usalama wao kutokana na kundi la Al Shabab.

Mwaka uliopita, serikali ya Kenya ilitangaza kufunga kambi hiyo kwa sababu za kiusalama baada ya kundi la Al Shabab kuendeleza mashambulizi katika maeneo kadhaa nchini humo.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Kenya, likiwemo lile la Amnesty International lilikwenda Mahakamani kutaka uamuzi huo kusitishwa kwa sababu ulikuwa kinyume cha katiba na ulikuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Umoja wa Mataifa pia umekuwa ukitaka Kenya kusitisha uamuzi wa kufunga kambi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.