Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yaendelea Hong Kong

Mamia ya waandamanaji katika uwanja wa ndege wa Hong Kong wametumia mashine ya kukata tiketi na mapipa ya kutupa taka, kuziba maeneo ya uwanja huo, katika makabiliano na maafisa wa usalama.

Waandamanaji kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong, Agosti 14, 2019.
Waandamanaji kwenye uwanja wa ndege wa Hong Kong, Agosti 14, 2019. C. Paget/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mwezi mmoja sasa, waandamanaji wamekuwa wakipiga kambi katika uwanja huo kuendelea kuonesha hasira zao dhidi ya uongozi wa Hong Kong, kupitisha sheria itakayowataka watu kufunguliwa mashtaka nchini China.

Uongozi wa Hong Kong ambao kwa sasa umesitisha kupitisha sheria hiyo, unahofia kuwa kuendelea kwa maandamano haya, kutaharibu uchumi wa eneo hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameeleza sababu kuu za mabadiliko na uingiliaji wa nguvu za nje wa hali ya Hong Kong, na kusisitiza kuwa, mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China ambayo hayaruhusiwi kuingliwa na nguvu za nje.

Maelezo hayo ameyatoa baada ya kuulizwa na wenzake wa Korea Kusini na Japan kuhusu hali ya Hong Kong na kueleza wasiwasi wao juu ya usalama wa wananchi wao mkoani humo.

Bw. Wang amesema serikali kuu ya China inaendelea kuunga mkono utawala wa serikali ya Hong Kong kwa mujibu wa sheria, kuunga mkono kithabiti polisi wa Hong Kong kutekeleza sheria kwa hatua madhubuti, na kuunga mkono kithabiti idara ya sheria ya Hong Kong kuwaadhibu kisheria wahalifu wanaojihusisha na vurugu za kimabavu. Pia itaendelea kutekeleza sera ya China Moja na Mifumo Miwili na kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong.

Bw. Wang pia amesema, anaamini serikali ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong itahakikisha haki halali za wageni mkoani humo na kutarajia pande zote kuunga mkono na kufuata msimamo wa haki juu ya serikali ya Hong Kong kupambana na vurugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.