Pata taarifa kuu
HONG KONG-USALAMA

Hong Kong: Beijing yalaani vitendo vya kigaidi, Trump aingilia kati

China imeshtumu shambulio la "ugaidi" dhidi ya raia wake wakati wa makabiliano Jumatano huko Hong Kong, mzozo ambao Donald Trump anatarajia kuona Beijing ikichukuwa hatu za "ubinadamu", kwa sababu ya mazungumzo ya biashara kati ya nchi hizo mbili.

Maafisa wa polisi wakipiga doria katika eneo la wa wasafiri katika uwanja wa ndege wa Hong Kong.
Maafisa wa polisi wakipiga doria katika eneo la wa wasafiri katika uwanja wa ndege wa Hong Kong. REUTERS/Thomas Peter
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wake alioandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Donald Trump, ameweka shinikizo kwa China, akitaja mambo mawili yanayotakiwa kushughuliwa haraka sana: suala la kidiplomasia (mzozo katika Hong Kong) na uchumi (mazungumzo ya biashara).

"Nchini China, mamilioni ya ajira hupotea na kwenda katika nchi ambazo hazitozi kodi baadhi ya bidhaa. Makampuni mengi yamefunga milango nchini China. Kwa ukweli ikiwa China inataka kufikia makubaliano (na Marekani) kwanza wachukuwe hatua za kibinadamu huko Hong Kong! ", Donald Trump ameonya.

Muda kidogo baadaye, kwenye ujumbe mwngine, alihakikisha kwamba Rais wa China Xi Jinping anaweza kuonyesha ubinadamu huo.

"Sina shaka kuwa ikiwa Rais Xi anataka kusuluhisha haraka na kwa ubinadamu mgogoro huko Hong Kong, hilo anaweza kufanya," Trump amesema.

Wakati huo idadi ya waandamanaji katika uwanja mkuu wa ndege mjini Hong Kong imepungua hadi chini ya watu 100 jana Jumatano, ikiwa ni matokeo ya marufuku iliyotolewa na mahakama dhidi ya waandamanaji kuukalia uwanja huo.

Hata hivyo ulinzi mkali bado umeimarishwa na abiria wanaotumia usafiri wa treni uliopo ndani ya uwanja huo wakitakiwa kuonesha tikiti kabla ya kuruhusiwa kuingia kwenye majengo ya uwanja wa ndege.

Waandamanaji walifurika na kudhibiti sehemu ya uwanja wa ndege wa Hong Kong kwa siku tano mfululizo hatua iliyosababisha kufutwa kwa mamia ya safari za ndege na kuzusha makabiliano kati ya waandamanaji na polisi wa kutuliza fujo.

Mapema Jumatano baadhi ya waandamanaji waligawa vipeperushi kwa watalii kuwataka radhi kwa kuchelewesha safari zao, jambo lililozusha mvutano kati ya waandamanaji na wasafiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.