Pata taarifa kuu
URUSI - MAREKANI

Rais Putin asema uhusiano wa nchi yake na Marekani umedorora

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema uhusiano kati ya nchi yake na Marekani umedorora chini ya rais Donald Trump.

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Urusi ameongeza kuwa kinachotokea sasa kinaonesha wazi kuwa uaminifu kati ya Moscow na Washington DC hasa kuhusu ushirikiano wa kijeshi, umeshuka sana.

Kauli ya Putin imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson akiwa jijini Moscow kuzungumza na mwenyeji wake Sergei Lavrov kuhusu mzozo wa Syria.

Uhusiano wa Marekani na Urusi ambao mwanzoni mwa mwaka huu ulionekana kuimarika baada ya kuapishwa kwa rais Trump ambaye alionekana kumsifia Putin, umeonekana kuyumba baada ya shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70 wakiwemo watoto.

Marekani imeishutumu Urusi kwa kushindwa kuizua Syria kutekeleza shambulizi hilo, na kuonya kuwa hali itakuwa mbaya ikiwa shambulizi hilo litajirudia tena.

Urusi imeendelea kusisitiza kuwa itaendelea kuiunga mkono serikali ya rais Bashar Al Assad na kulaani hatua ya Marekani kushambulia uwanja wa ndege wa kijeshi na kuharibu ndege za Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.