Pata taarifa kuu
G7-SYRIA-URUSI

Mataifa ya G7 yashindwa kukubaliana kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na Syria

Mataifa ya G7 yaliyoendelea kiviwanda duniani yameshindwa kuafikiana kuhusu kuiwekea vikwazo Urusi na Syria baada ya shambulizi la silaha za kemikali dhidi ya raia wa Syria wiki iliyopita.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani  Rex Tillerson na mwenzake wa Uingereza  Boris Johnson katika mkutamo wa G7 mjini Lucca nchini Italia APrili 11 2017
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson na mwenzake wa Uingereza Boris Johnson katika mkutamo wa G7 mjini Lucca nchini Italia APrili 11 2017 REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya nje wa Mataifa hayo, wamekuwa wakijaribu kutafuta mwafaka kuhusu vikwazo hivyo bila mafanikio nchini Italia.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amekwenda nchini Urusi kwenda kuishawishi serikali hiyo kuacha kuiunga mkono serikali ya Syria bila ya mwafaka kutopatikana.

Hata hivyo, mataifa hayo yamekubaliana kwa kauli moja  kuwa amani ya kudumu haiwezi kupatikana nchini Syria ikiwa rais Bashar Al Assad ataendelea kuwa madarakani.

Pendekezo la kuiwekea Syria na Urusi vikwazo vipya ilikuwa imependekezwa na Uingereza.

Marekani ambayo imetetea uamuzi wake wa kushambulia silaha za kivita za jeshi la Syria wiki iliyopita, imeonya kuwa haitakubali tena silaha za kemikali kutumiwa kuwashambulia raia wa kawaida.

Serikali ya Syria ikiungwa mkono na mshirika wake Urusi, imesema Damascus haikutekeleza shambulizi hilo kama inavyodaiwa.

Watu zaidi ya 70 wakiwemo watoto walijeruhiwa katika shambulizi hilo baya katika nchi hiyo ambayo imekuwa kwenye vita tangu mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.