Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-URUSI-KOREA KASKAZINI

Bunge la Marekani laidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran

Bunge la wawakilishi nchini Marekani limepiga kura kuwekwa kwa vikwazo vipya dhidi ya nchi ya Iran, Korea Kaskazini na Urusi, uamuzi ambao huenda ukazidisha sintofahamu kati ya nchi hiyo na Urusi.

Bunge la Marekani laidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini. Katika Picha rais Putin akiwa na rais Trump
Bunge la Marekani laidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini. Katika Picha rais Putin akiwa na rais Trump newsoftheworld
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu uliofikiwa na wabunge sasa utamzuia rais Donald Trump kuwa na uwezo wa kuondoa adhabu yoyote dhidi ya mataifa hayo.

Vikwazo hivi ambavyo kura yake imepitishwa na wabunge 419 imefanyika baada ya majuma kadhaa ya majadiliano.

Spika wa bunge Paul Ryan amesema kuwa nchi yake ni lazima ichukue hatua madhubuti kwaajili ya kulinda usalama wake ulioko hatarini kuchezewa na mataifa hayo.

Hatua hizi sasa zitasubiri baraka za bunge las Seneti ambako wabunge wengi wanaunga mkono kuwekwa kwa vikwazo hivyo ingawa wanataka hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya Korea Kaskazini.

Muswada huu uliopitishwa ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita yanayolenga kuiadhibu nchi ya Urusi kwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana pamoja na nchi hiyo kuchukua eneo la Crimea nchini Ukraine.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje wa Marekani, Ed Royce amesema kuwa "chini ya utawala wa Vladmir Putin, Urusi imeivamia nchi ya Ukraine, kuchukua maeneo yake na kuidhoofisha Serikali."

Hata hivyo muswada huu huenda ukawa na madhara pia kwa mataifa ya Ulaya ambayo baadhi ya mashirika yake yanategemewa kwa maendeleo ya gesi ya Urusi ambayo inasambazwa kwenye nchi nyingi za Ulaya.

Vikwazo vipya dhidi ya Iran vimelenga jeshi la nchi hiyo ambalo linatuhumiwa kufadhili makundi ya kigaidi na kwa nchi ya Korea Kaskazini ni kutokana na majaribio yake ya silaha za masafa marefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.