Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-USHIRIKIANO

Marekani yachukua vikwazo dhidi ya Iran

Marekani imeiwekea Iran vikwazo vipya vya kiuchumi kwa kuituhumu kukiuka kuvunja mkataba wa kimataifa kuhusu shughuli zake za nyuklia na mpango wake wa majaribio ya makombora ya masafa marefu kombora pamoja na kufanya "shughuli za uharibifu" katika Mashariki ya Kati.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameahidi kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa serikali na taasisi yoyote nchini Marekani waliochukua hatua dhidi ya wananchi wa Iran na mataifa mengine ya Kiislam katika ukanda huo."
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameahidi kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa serikali na taasisi yoyote nchini Marekani waliochukua hatua dhidi ya wananchi wa Iran na mataifa mengine ya Kiislam katika ukanda huo." Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Fedha imewachukulia hatua watu 18 na taasisi zinazotuhumiwa kusaidia kile ilichokiita "washirika wa Iran katika shughuli haramu za kimataifa au za kihalifu."

Kwa mujibu ya Wizara ya Fedha baadhi walishiriki katika kutengeneza ndege zisizokuwa na rubani na vifaa vya kijeshi, kutengeneza meli na kutoa huduma ya umeme kwa niaba ya jeshi au kwa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi.

Wengine walihusika katika wizi wa programu za kompyuta kutoka Magharibi" na kuziuza kwa serikali ya Iran.

"Marekani bado ina wasiwasi na shughuli za uharibifu za Iran katika Mashariki ya Kati, ambazo zindhoofisha usalama na ustawi wa ukanda huo," wizara ya Fedha imeandika katika taarifa yake na kuishtumu Iran kwamba inasaidia kundi la Hezbollah kutoka Lebanon, Hamas kutoka Palestina, Rais wa Syria Bashar al-Assad na waasi wa Houthi Shiite nchini Yemen.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameahidi kuwawekea vikwazo baadhi ya maafisa wa serikali na taasisi yoyote nchini Marekani waliochukua hatua dhidi ya wananchi wa Iran na mataifa mengine ya Kiislam katika ukanda huo."

Siku ya Jumatatu, utawala wa Donald Trump aliitoa uamuzi kuwa Tehran inaheshimu mkataba wa 2015 unaositisha shughuli zake za nyuklia kwa kubadilishana kuondoa vikwazo vya kimataifa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.