Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-USALAMA

Rohani afutilia mbali shutma za Trump na kulaani mtazamo wa Riyadh

Rais wa Iran Hassan Rohani alijibu siku ya Jumatatu, Mei 22 kufuatia mashambulizi ya Marekani na Saudi Arabia dhidi ya nchi yake, akilaani mkutano kati ya viongozi hao wawili siku ya Jumapili mjini Riadh, nchini Saudi Arabia.

Rais wa Iran Hassan Rohani, katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kuchaguliwa kwake tena mjini Tehran, Mei 22.
Rais wa Iran Hassan Rohani, katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kuchaguliwa kwake tena mjini Tehran, Mei 22. ATTA KENARE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Rohani ameuita mkutano huo "maonyesho"yasiokuwa na "thamani yoyote ya kisiasa" .

"Mkutano wa Saudi Arabia ulikuwa maonyesho yasiokuwa na thamani ya kisiasa, wala vitendo, Saudi Arabia tayari iliandaa maonyesho hayo katika siku za nyuma," alisema Hassan Rohani, katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu kuchaguliwa kwake tena Ijumaa, Mei 19 kwa awamu ya pili ya miaka minne.

Hassan Rohani alikana kuunga mkono ugaidi, tuhuma ambazo rais wa Marekani Donald Trump na Salman, Mfalme wa Saudi Arabia waliishtumu Iran wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Riyadh. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikualikwa katika mkutano huo na rais Trump aliomba mataifa yote "kujitenga" na Iran.

"Wale ambao waliunga mkono magaidi hawawezi kupambana dhidi yao"

"Wale ambao walipigana dhidi magaidi ni raia wa Iraq na Syria. Washauri wa kijeshi wa Iran waliwasaidia, na wataendelea kufanya hivyo, "alisema Hassan Rohani, ambaye pia alitetea kundi la Hezbollah.

"Wale ambao waliunga mkono magaidi hawawezi kupambana nao," kwa upande mwingine Bw. Rohani alishtumu. "Sidhani kwamba wananchi wa Marekani watasahau damu iliyomwagika Septemba 11," ameongeza rais Rohani, akimaanisha mashambulizi ya mwaka 2001 nchini Marekani, ambapo marubani 15 kati ya 19 ambao waliteka nyara ndege za Marekani na kua watu 3000 , walikua raia wa Saudi Arabia.

Pia alikosoa mkataba wa bilioni 110 uliofikia kati ya Washington na Riyadh kwa ajili ya ununuzi wa silaha. "Humuwezi kutatua tatizo la ugaidi tu kwa kutoa fedha kutoka wananchi wako kwa nchi kama Marekani," alisema rais wa Iran, akimaanisha Donald Trump.

"Hatutaomba ruhusa ya mtu yeyote" kwa ajili ya majaribio ya kombora

Pia alikataa kusitisha majaribio yoyote ya makombora kama ombi la Marekani na Saudi Arabia, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Tehran, Siavosh Ghazi. Rais Hassan Rohani alitangaza kwamba nchi yake itaendelea na majaribio yake ya makombora "kama itahitajika."

"Jueni kwamba wakati tutahitajika kufanya majaribio ya kiufundi ya makombora tutafanya na hatutaomba ruhusa kutoka kwa mtu yeyote," pia alisema rais wa Iran. "Makombora yetu ni kwa ajili ya ulinzi wetu na kwa amani, na wala hayatengenezwi kwa kutishia usalama wa mtu yeyote, " aaliongeza rais Hassan Rohani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.