Pata taarifa kuu
NICARAGUA-UCHUMI

Ujenzi wa mfereji mkubwa wapingwa Nicaragua

Ujenzi wa mfereji mkubwa utakaotoa maji kwenye bahari moja kwenda nyingine ukipitia nchini Nicaragua unatazamiwa kuanza hii Jumatatu Desemba 22.

Waandamanaji katika mji wa Manuaga, nchini Nicaragua, wakipinga ujenzi wa mfereji mkubwa katika bahari Desemba 10 mwaka 2014.
Waandamanaji katika mji wa Manuaga, nchini Nicaragua, wakipinga ujenzi wa mfereji mkubwa katika bahari Desemba 10 mwaka 2014. REUTERS/Oswaldo Rivas
Matangazo ya kibiashara

Ujenzi huo utasimamiwa na kampuni kutoka China. Mfereji huo ni mrefu na mpana kuliko ule wa Panama. Inaaminiwa kuwa mfereji huo utaingiza asilimia 5 ya mapato yanayotokana na biashara duniani. Lakini licha ya kuwa mradi huo utakua na manufaa makubwa kwa uchumi wa Nicaragua, raia wameupokea kwa shingo upande.

"Wachina nje". Hii ni kauli iliyokua ikitolea na maelfu ya raia wa Nicaragua waliokua wakiandamana wakipinga dhidi ya ujenzi wa mfereji, ambao utakua na urefu wa kilomita 280. Waandamanaji hao wamekosoa utaratibu uliyotumiwa kwa kutoa zabuni hiyo kwa kampuni kutoka China (HK Nicaragua Canal Development).

"Mradi huo wa uwekezaji unaweza kukamilika pamoja na mlolongo wa faida za ajabu! Kwa mfano, hakuna kodi za ndani zitakazolipwa, hakuna kodi zitakayolipwa kwa serikali kuu", amelani Victor Hugo Tinoco, mbunge kutoka chama cha MRS (Movimiento Renovador Sandinista).

Sheria inaipa kampuni hiyo kutoka China miaka 50 ya kuendesha shughuli zake mbadala nchini Nicaragua ambayo itaweza ikaongezwa kwa kipindi fulani. Sheria hiyo inaipa pia kampuni hiyo kutoka china uhuru wa ujenzi wa viwanja vya ndege, maeneo muhimu pamoja na maeneo ya kitalii hususan hoteli.

" Serikali ya Nicaragua hakuna itakachowekeza katika shughuli hizo zitakazo endeshwa na kampuni hiyo kutoka China, lakini itakua ikitoa ardhi. Hata hivyo mkataba unaeleza kwamba Nicaragua itapata asilimia 1 ya thamani ya hisa na katika miaka 50 itakuwa na asilimia 51 ya htamani ya hisa", anasema Manuel Coronel Kautz, mwenyekiti wa mamlaka inayosimamia mradi wa ujenzi wa mfereji huo.

Ujenzi wa mfereji mkubwa utakaotoa maji kwenye bahari moja kwenda nyingine ukipitia nchini Nicaragua.
Ujenzi wa mfereji mkubwa utakaotoa maji kwenye bahari moja kwenda nyingine ukipitia nchini Nicaragua. Worl Obsever

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.