Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Johnson: Hakuna mpango wowote mbadala kuhusu Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anawasilisha mapendekezo mapya kwa uongozi wa Umoja wa Ulaya jijini Brussels, kuelezea hatima ya nchi yake baada ya kujiondoa kwenye Umoja huo, huku dalili zikionesha kuwa huenda ikaondoka bila mkataba.

Boris Johnson na Jean-Claude Juncker baada ya mkutano wao, Septemba 16, 2019.
Boris Johnson na Jean-Claude Juncker baada ya mkutano wao, Septemba 16, 2019. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Ulaya inasema itatazama kwa makini mapendekezo hayo kabla ya kutoa mtazamo wake.

Wabunge nchini Uingereza wamekwamisha juhudi za serikali nchini humo kwa nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja huo bila mkataba.

Mapema hivi leo, Johnson akihotubia mkutano wa chama cha Conservative mjini Manchester, amesisitiza kuwa ni lazima nchi hiyo ijiondoe kwenye Umoja wa Ulaya, ifikapo tarehe 31 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.