Pata taarifa kuu

Urusi: Mamake Alexeï Navalny akabidhiwa mwili wa mwanawe

Baada ya majuma mawili ya mvutano na mamlaka ya Urusi, hatimaye mamake Alexeï Navalny ameweza kupokea mwili wa mwanawe. Tangazo hilo lilitolewa kwenye mitandao na timu ya wapinzani, ambayo imefafanua kuwa bado haijajua ni wapi na chini ya mazingira gani mazishi ya Bwana Navalny yatafanyika.

Bango lenye picha ya Alexeï Navalny, aliyefariki katika gereza la Arctic nchini Urusi, Jumamosi hii Februari 24, 2024 katikati mwa Milan, Italia.
Bango lenye picha ya Alexeï Navalny, aliyefariki katika gereza la Arctic nchini Urusi, Jumamosi hii Februari 24, 2024 katikati mwa Milan, Italia. AFP - GABRIEL BOUYS
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Moscow, Jean-Didier Revoin

Hii bila shaka ni ahueni kwa walio karibu naye. Mamlaka hatimaye imekubali kukabidhi mwili wa Alexeï Navalny kwa mama yake.

Kulingana na msemaji wa kiongozi huyu wa upinzani, Lyoudmila Navalnaïa bado yuko Salekhard kuchukua mwili wa mtoto wake. Lakini katika hatua hii, Kira Yarmish amefafanua kwamba bado hajui ikiwa viongozi watazuia mazishi kufanyika kama familia inavyotaka na kama Alexei Navalny anastahili.

Siku mbili zilizopita, Lyoudmila Navalnaïa alirusha video mitandaoni akishutumu uhuni unaofanywa na mamlaka. Alibaini kwamba walitaka kumkabidhi mwili wake kwa sharti tu kwamba mazishi ya mwanawe yafanyike kwa siri.

Bado hakuna habari iliyovuja juu ya uwezekano wa makubaliano kati ya mamlaka na mama wa kiongozi huyo wa upinzani. Mara moja, timu nzima ya Alexeï Navalny, ambayo inaishi uhamishoni nje ya Urusi, inawashukiru kwenye mitandao makumi ya maelfu ya watu ambao walimtolea wito hadharani Vladimir Putin ili mwili wa Bw. Navalny ukabidhiwe familia yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.