Pata taarifa kuu

Imamu wa Tunisia aliyetimuliwa anataka kuchukua hatua za kisheria kurejea Ufaransa

Imamu wa Tunisia, aliyefukuzwa siku ya Alhamisi na mamlaka ya Ufaransa ambapo mamlaka ilimtuhumu kwa kutoa matamshi ya chuki, ameshutumu uamuzi uliochukuliwa "kiholela" siku ya Ijumaa na kutangaza kwamba atachukua hatua za kisheria kuubatilisha na kurejea kwa familia yake.

Imam wa Tunisia Mahjoub Mahjoubi akizungumza nyumbani kwake Februari 23, 2024, siku moja baada ya kufukuzwa nchini Ufaransa.
Imam wa Tunisia Mahjoub Mahjoubi akizungumza nyumbani kwake Februari 23, 2024, siku moja baada ya kufukuzwa nchini Ufaransa. © Fethi Belaid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Imamu wa mji mdogo wa Bagnols-sur-Cèze ulioko kusini mwa Ufaransa, Mahjoub Mahjoubi alikamatwa na kisha kufukuzwa siku ya Alhamisi hadi Tunisia ambako aliwasili muda mfupi kabla ya saa sita usiku ndani ya ndege kutoka Paris.

Imamu huyo anaishi Ufaransa tangu katikati ya miaka ya 1980, ni mume na baba wa watoto watano, alikuwa anawindwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Gérald Darmanin, ambaye aliomba siku ya Jumapili kunyang'anywa kibali chake cha kuishi nchini Ufaransa.

Mahjoub Mahjoubi alishutumiwa haswa kwa kurusha video ambayo alielezea "bendera ya rangi tatu" - bila kutaja kama ni bendera ya Ufaransa - kama "bendera ya kishetani" ambayo "haina thamani kwa Allah" (Mwenyezi Mungu kwa Kiarabu).

Alijitetea akisema "kuteleza kwa ulimi", akieleza kwamba alikuwa akikemea uhasama kati ya mashabiki wa wa timu kutoka nchi za Maghreb wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) hivi majuzi. "Nitapigana kurejea Ufaransa ambako nimeishi kwa miaka 40," Imamu huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kutoka mji wa Soliman, yapata kilomita thelathini mashariki mwa mji mkuu wa Tunis.

"Wakili wangu atachukua hatua za kisheria nchini Ufaransa na ikiwa mahakama haitanitendea haki, nitakata rufaa, na kisha nitakata rufaa katika Mahakama ya Ulaya" ya haki za binadamu, ameongeza. "Sikuitukana jamii ya Kiyahudi au bendera ya Ufaransa," ameongeza imam huyo, mwenye umri wa miaka 52, ambaye mke wake na watoto wake watano ni raia wa Ufaransa.

Bw. Darmanin alithibitisha siku ya Alhamisi kwenye ukurasa wake wa X " kwamba kufukuzwa kwa Imam huyo kumetokana na sheria mpya ya uhamiaji ambayo imeidhinishwa hivi karibuni nchini Ufaransa, bila sheria hiyo, uamuzi huo wa kufukuzwa haungekuwa rahisi na haraka, sheria ambayo inaifanya Ufaransa kuwa na nguvu zaidi. "Uthabiti ndio kanuni," aliongeza waziri huyo, akimlaumu "imamu mwenye msimamo mkali na matamshi yasiyokubalika".

"Kufukuzwa kwangu kulitokana na uamuzi wa kiholela wa Waziri wa Mambo ya Ndani. Bw. Darmanin anajaribu kuzua gumzo kuhusu sheria ya uhamiaji kwa kumtumia Mahjoub Mahjoubi," amejibu imamu katika taarifa yake kwa shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.