Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Uturuki: PKK yadai shambulio la kujitoa mhanga mjini Ankara

Mlipuko mkubwa ulipiga Jumapili Oktoba 1 asubuhi katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, karibu na Bunge. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki imesema ni "shambulio la kigaidi" lililofanywa na watu wawili. Mmoja alikufa wakati akitoa kilipuzi chake, mwingine alipigwa risasi. Maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa kidogo. Saa kadhaa baadaye, waasi wa Kikurdi wa PKK walidai kuhusika na shambulio hilo.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza na wabunge mjini Ankara tarehe 1 Oktoba 2023, saa chache baada ya kutokea mlipuko uliosababisha watu wawili kujeruhiwa katika mji mkuu.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza na wabunge mjini Ankara tarehe 1 Oktoba 2023, saa chache baada ya kutokea mlipuko uliosababisha watu wawili kujeruhiwa katika mji mkuu. via REUTERS - MURAT CETINMUHURDAR/PPO
Matangazo ya kibiashara

"Magaidi wawili walionekana kwenye gari jepesi la kibiashara karibu saa 9:30 asubuhi (sawa na saa 6:30 asubuhi kwa saa za ulimwengu) mbele ya lango la kuingilia la Kurugenzi Kuu ya Usalama ya Wizara yetu ya Mambo ya Ndani na kutekeleza shambulio la bomu ", imebaini wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo imebainisha kuwa maafisa wawili wa polisi "walijeruhiwa kidogo" na moto uliosababishwa a mlipuko huo.

"Mmoja wa magaidi alijilipua na mwingine akaangamizwa," inaongeza wizara kwenye X (zamani ikiitwa Twitter). Kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki, urushanaji risasi pia ulisikika katika eneo hilo kunakopatikana makao makuu ya Bunge, ambako kunapatikana pia ofisi za wizara nyingi. Magari mengi ya polisi na ambulansi zilitumwa  katika eneo hilo.

Kitongoji ambacho shambulio lililotekelezwa na watu wawili huko Ankara, Uturuki, kilizingirwa mnamo Oktoba 1, 2023.
Kitongoji ambacho shambulio lililotekelezwa na watu wawili huko Ankara, Uturuki, kilizingirwa mnamo Oktoba 1, 2023. REUTERS - CAGLA GURDOGAN

"Magaidi hawataweza kufikia malengo yao," amesema Erdogan

"Bado hakuna taarifa juu ya utambulisho wa wahusika wa shambulio hilo, wala madai yoyote kwa sasa. Shambulio hilo lilifanyika katika eneo lililolindwa sana la mji mkuu, ambalo linalindwa zaidi.

Mji mkuu wa Uturuki, kama vile mji mkuu wa Istanbul, ulikumbwa na mfululizo wa mashambulizi mabaya mwaka 2015 na 2016, yaliyohusishwa na waasi wa Kikurdi au kundi la Islamic State.

Mwanzoni mwa alasiri, rais wa Uturuki alihutubia Bunge kama ilivyopangwa. Alituma ujumbe wa wazi kwa "mafisadi wanaotishia amani na usalama wa raia". "Magaidi hawajafikia malengo yao na kamwe hawataweza kuyafikia," alisisitiza Recep Tayyip Erdogan.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.