Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Uturuki: Watu zaidi ya 5 wafariki

Nairobi – Takriban watu 5 wameripotiwa kufa nchini Uturuki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.Maeneo yaliyoathirika pakubwa ni Instanbul  na sehemu za kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.

Magari zaidi yakwama kwenye mafuriko jijini Instabul-Uturuki
Magari zaidi yakwama kwenye mafuriko jijini Instabul-Uturuki AP - Sercan Ozkurnazli
Matangazo ya kibiashara

Picha zinazosambaa mtandaoni zinaonyesha majumba yaliyoharibiwa na hata magari kukwama kwenye maji.

Huduma ya dharura ya Uturuki imesema watu watatu pia walifariki siku ya Jumanne na watatu walipotea katika mafuriko yaliyokumba mji wa kaskazini magharibi wa Kirklareli.

Mvua hizo zimekuja baada ya msimu wa kiangazi ambao ulishuhudia mabwawa ya maji ya jiji lenye watu milioni 16 yakishuka hadi kupungua kwa miaka tisa.

Wanasayansi wengi wanabaini kwamba hali hiyo ni kutokana na uhusiano kati ya ongezeko la joto ulimwenguni linalosababishwa na shughuli za binadamu na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa.

Uturuki imekuwa eneo la majanga kadhaa ya asili katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na vipindi vya ukame mkali na moto mkali wa misitu mwishoni mwa mwezi Julai na mapema mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.