Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Ufaransa: watu wawili wauawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulio la risasi Marseille

Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na wa tatu kujeruhiwa siku ya Alhamisi jioni, Septemba 28, baada ya kufyatuliwa risasi katika vitongoji vyenye wakaazi kaskazini mwa mji wa Marseille, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu maafisa wa Zima moto na vyanzo vya polisi.

Watu wawili wameuawa huko Chutes-Lavie, katika eneo la 4 la Marseille, Ufaransa.
Watu wawili wameuawa huko Chutes-Lavie, katika eneo la 4 la Marseille, Ufaransa. © Nicolas Tucat / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili litokea karibu saa moja na dakika arobaini (saa za Ufaransa) huko Chutes-Lavie, katika eneo la 4 la Marseille, kulingana na vyanzo hivi. "Mhalifu, aliyejihami kwa silaha ndefu, alikimbia" kwa gari, chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP.

Taarifa zaidi zinakujia...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.