Pata taarifa kuu

Balozi wa Ufaransa ameondoka Niger, baada ya wiki kadhaa za mvutano

Balozi wa Ufaransa, Sylvain Itté ameondoka Niger nchini Niger Jumatano, Septemba 27, na atarejea kuwasili saa chache zijazo. Siku ya Jumapili jioni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kuwa balozi Sylvain Itté ataondoka nchini Niger hivi karibuni. aliyasema hayo wakati wa mahojiano ya televisheni, wakati ambapo mwanadiplomasia na maafisa kadhaa wa timu yake walikuwa wakiishi katika ubalozi tangu kufanyika kwa mapinduzi mwishoni mwa mwezi Julai.

Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Agosti 28, 2023.
Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Agosti 28, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Sylvain Itté ameondoka Niger. Balozi wa Ufaransa ameondoka Niamey siku ya Jumatano kuelekea Ndjamena, mji mkuu wa Chad, ambapo mwanadiplomasia huyo ataanzisha safari yake kwenda Paris.

Kuondoka huku kunaashiria mwisho wa wiki kadhaa za mvutano kati ya Paris na wanajeshi iwalioko madarakani huko Niamey. Utawala wa kijeshi ulimtangaza balozi wa Ufaransa kuwa mtu wasiyemtaka mwishoni mwa mwezi wa Agosti. Tangu wakati huo, Sylvain Itté amekuwa akiishi pamoja na maafisa sita wa timu yake katika ubalozi unaofuatiliwa kwa karibu na wanajeshi wa Niger.

'Mateka'

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alibaini kwamba balozi Sylvain Itté anashikiliwa "mateka" na jeshi lililoko madarakani ambalo lilikuwa likizuia balozi wa Ufaransa na wasaidizi wake kupeanwa chakula.

Ikiwa mwanzoni serikali ya Ufaransa ilitangaza kumbakiza kwenye wadhifa huo, hatimaye Paris ilirejelea kauli yake Jumapili Septemba 24. Emmanuel Macron alibaini kwamba balozi huyo atarejea Ufaransa "katika saa zijazo".

Pia alitangaza kwamba wanajeshi 1,500 wa Ufaransa waliotumwa Niamey wataondoka katika ardhi ya Niger ifikapo mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.