Pata taarifa kuu

Balozi kadhaa zapunguza wafanyakazi wao kutokana na uwezekano wa Niger kuvamiwa kijeshi

Nchini Niger, ni katika muktadha wa uingiliaji kati kijeshi unaowezekana ambapo suala la usalama wa wafanyakazi wa kidiplomasia linaibuka. Balozi kadhaa zimeamua kupunguza wafanyakazi wao.

Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango kutoka Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Julai 30, 2023.
Waandamanaji wakiwa wameshikilia bango kutoka Ubalozi wa Ufaransa mjini Niamey, Julai 30, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kupunguzwa kwa idadi ya wafanyakazi kwenye mabalozi ya nchi za kigeni waliopo nchini Niger kumekuwa kwa kiwango kikubwa. Balozi za Marekani, Ujerumani au hata Wafaransa zimeamua kupunguza wafanyakazi wao. Baadhi ya balozi bado zinasuiri kuchukuwa uamuzi kama huo. Maafisa kwenye balozi kadhaa ambao walikuwa wamekwenda likizo hawajarejea nchini Niger, wengine ambao walikuwa wamemaliza mkataba wao wa kutumikia nchini Niger nafasi zao zitasalia tupu.

Idadi ya wafanyakazi yapunguzwa

Balozi kadhaa, ambazo wakati mwingine zilikuwa na maafisa zaidi ya mia moja, hazina zaidi ya kumi. zingine zilikuwa tayari zikifanya kazi na timu ndogo sana na kujikuta zikiwa na karibu balozi mmoja. Mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Ufaransa, mwishoni mwa mwezi wa Julai, na matamshi yaliyotumiwa na viongozi wa mapinduzi yalizua wasiwasi. "Sitaki wafanyakazi wetu wawe na shida yoyote, kwa hivyo nimeomba wafanyakazi wasio wa lazima kuondoka na kufanya kazi wakiwa nyumbani ," mwanadiplomasia mmoja amesema.

Hofu ya kufukuzwa

Kwa mabalozi kadhaa, hofu ya kufukuzwa nchini pia ipo. Kuhusu shughuli, pia imepunguzwa, kufuatia kusimamishwa kwa programu za ushirikiano. Kuhusu raia wa kigeni, wanaendelea kuondoka. Jana, Jumanne Agosti 8, watu kumi na wanne, raai wa Ufaransa, kwa mfano, waliondoka nchini Niger. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuondoka kwa takriban raia 100 siku ya Ijumaa. "Wale wanaotaka kuondoka wanapaswa kujiandikishe na tutawasaidia," amesema Mathew Miller, msemaji wa diplomasia ya Marekani, akiongeza kuwa kusimamishwa kwa misaada ya maendeleo na ushirikiano wa usalama kunaweza kuondolewa haraka sana ikiwa utaratibu wa kikatiba umerejeshwa na mamlaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.