Pata taarifa kuu

Balozi wa Ufaransa ameondoka nchini Niger

Nairobi – Balozi wa Ufaransa nchini Niger, ameondoka kwenye taifa hilo ikiwa ni mwezi moja tangu uongozi wa kijeshi kumtaka kuondoka.

Paris ina wanajeshi 1,500 nchini Niger ambao wamekuwa wakisaidia katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi
Paris ina wanajeshi 1,500 nchini Niger ambao wamekuwa wakisaidia katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Uhusiano kati ya Ufaransa na Niger ulionekana kuharibika baada ya wanajeshi kwenye taifa hilo la Afrika kumuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia Mohamed Bazoum mwezi Julai.

Ufaransa kwa upande wake imekataa kutambua uongozi mpya wa kijeshi nchini Niger na ilikuwa imepuuza wito wa jeshi kutaka kumuondoa balozi wake jijini Niamey.

Wanajeshi wa Niger wameonekana kupuuza wito wa kurejesha utawala wa kiraia
Wanajeshi wa Niger wameonekana kupuuza wito wa kurejesha utawala wa kiraia © Stringer / Reuters

Hatua kuodoka kwa balozi Sylvain Itté inakuja siku chache baada ya rais Emmanuel Macron kutangaza kuwa ataondoka.

Katika taarifa yake, rais Macron pia alitangaza kwamba nchi yake itawaondoa wanajeshi wake nchini Niger kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Paris ina wanajeshi 1,500 nchini Niger ambao wamekuwa wakisaidia katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.