Ukraine: Ukraine yadai kudungua ndege zisizo na rubani juu ya anga ya mji mkuu
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine wameangusha zaidi ya ndege 20 zisizo na rubani za Urusi zilizokuwa zikilenga mji mkuu wa Ukraine, Kiev siku ya Jumapili alfajiri, imetangaza mamlaka nchini Ukraine, ambayo imeripoti mtu mmoja kujeruhiwa na vifusi vilivyoanguka.
Imechapishwa:
Kwa sasa kumekuwa na vita vya maneno kati ya nchi hizi mbili hasimu. Kila nchi imekuwa ikidai kuangusha ndege za upande mwingine bila hata hivyo kutoa ushahidi tosha.
Vita vya Urusi nchini Ukraine sasa vimedumu zaidi ya mwaka mmoja, tangu mwezi Februari, tarehe 24 mwaka 2022.
Hata hivyo nchi zote mbili zinaendelea kupoteza katika vita hii visiokoma, huku kila upande ukiwa na washirika wanaousaidia katika vita hivi.
Majaribio ya kusitishwa kwa vita hivyo yamegonga mwamba mara kadhaa, huku baadhi ya nchi zikidai kujaribu kusuluhisha mgogoro huo bila mafaanikio.