Pata taarifa kuu

NATO yasema Ukraine inapiga hatua katika vita dhidi ya Urusi

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg amesema kuna ishara kuwa mabaki ya ndege zisizokuwa na rubani zilizopatikana katika ardhi ya Romania, zilirushwa kwa makusudi na Urusi.

Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jeshi la nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg © Alexandru Dobre / AP
Matangazo ya kibiashara

Stoltenberg amesema kitendo hicho kimetishia usalama wa mwanachama wake na kinapaswa kulaaniwa.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo wa NATO ameeleza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kusonga mbele na kuchukua maeneo yaliyokuwa yamechukuliwa na jeshi la Urusi, licha ya kuendelea kushuhudia vita vigumu.

Siku chache zilizopita, jeshi la Ukraine limekuwa likisema limepata mafanikio kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Urusi katika maeneo ya Kusini mwa nchi yake, baada ya kupokea silaha zaidi za kijeshi na fedha kutoka kwa washirika wake.

Wakati hayo yakijiri, ndege za Urusi zisizokuwa na rubani zimeendelea kulenga na kuharibu miundo mbinu muhimu hasa ghala la kuhifadhu nafaka katika jimbo la Odesa nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.