Pata taarifa kuu

Romania ina wasiwasi kuhusu milipuko ya mabomu ya Urusi karibu na mpaka wake

Urusi imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo la kusini-magharibi mwa Ukraine linalopakana na Romania, ambako bandari na miundombinu mingine muhimu ya mauzo ya nafaka vinapatikana.

Rais wa Romania Klaus Iohannis, Julai 20, 2020.
Rais wa Romania Klaus Iohannis, Julai 20, 2020. AP - Stephanie Lecocq
Matangazo ya kibiashara

Tangu kusitishwa mwezi Julai kwa makubaliano yaliyoiwezesha Ukraine kusafirisha nafaka zake nje ya nchi kupitia Bahari Nyeusi, Urusi imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo la kusini magharibi mwa Ukraine linalopakana na Romania, ambako kuna bandari na miundombinu mingine muhimu kwa biashara hii.

Siku ya Jumatatu, Ukraine ilidai kuwa na ushahidi kwamba ndege zisizo na rubani za Urusi zilianguka usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu nchini Romania. Bucharest alikanusha madai haya.

Lakini Rais Klaus Iohannis hafichi wasiwasi wake. Amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa Luxembourg Xavier Bettel:

"Hakuna mabaki, hakuna ndege zisizo na rubani na hakuna kifaa chochote kilichoingia nchini Romania. Tuna udhibiti kamili wa ardhi yetu. Tumekagua kila kitu na ninaweza kuwahakikishia raia. Hakuna ndege yoyote iliyoingia nchini Romania. Lakini ndio, tuna wasiwasi kwa sababu mashambulizi haya yanafanyika umbali mfupi sana kutoka mpaka wa Romania. Leo tu, Waziri wetu wa Ulinzi ameniambia kuhusu mashambulizi ambayo yalithibitishwa mita 800 kutoka mpaka wetu. Kwa hiyo ni karibu sana tena sana. "

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.