Wahamiaji wanne wamezama nchini Ugiriki
Wahamiaji wanne wameuwa katika ajali ya boti katika visiwa vya Lesbos nchini Ugiriki wengine 18 wakiwa wameokolewa.
Imechapishwa:
Waliookolewa walipelekwa katika eneo la Mytilene, mji mkuu wa Lesbos, eneo kuu ambalo wahamiaji hutumia wakitokea nchini Uturuki.
Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu uraia wa wahamiaji hao na hali ya kiafya ya waliookolewa.
Mwezi Juni, boti ya uvuvi iliyokuwa imejaa wahamiaji zaidi ya 750 wakitokea nchini Libya ilizama ikielekea nchini Ugiriki.
Karibia wahamiaji 100 waliookolewa na ilidaiwa kuwa wengine 600 walizama kwa mujibu wa takwimu kutoka Ugiriki.
Maelfu ya wahamiaji wengi wakitokea nchini Syria, Afghanistan na Pakistan, wameripotiwa kuingia nchini Ugiriki wakitumia bahari na maeneo ya mpaka na Uturuki.
Kutokana na sheria kali kuhusu uhamiaji, Ugiriki imeimarisha uchunguzi katika bahari kwenye mpaka wake na Uturuki.