Pata taarifa kuu

Ukraine: Watu Saba wauawa katika shambulio la Urusi

Watu saba wameuawa katika shambulio la kombora la Urusi katika mji wa Chernihiv kaskazini mwa Ukraine, saa chache baada ya rais Vladimir Putin kukutana na makamanda wa ngazi ya juu katika jeshi.

Jeshi la Urusi lilipitia jiji hilo lilipovamia Ukraine kupitia Belarus mnamo Februari 2022, kabla ya kuzuiwa na vikosi vya Kyiv
Jeshi la Urusi lilipitia jiji hilo lilipovamia Ukraine kupitia Belarus mnamo Februari 2022, kabla ya kuzuiwa na vikosi vya Kyiv © National Police/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Chernihiv, unaopatikana kilomita 150 kaskazini mwa mji wa Kyiv kuelekea nchini Belarus, haujakuwa ukishuhudia mashambulio tangu Urusi kuivamia Ukraine.

Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika baadhi ya miji ya mashariki na kusini mwa Ukraine ambako pia uharibifu mkubwa umeripotiwa.

Jeshi la Urusi lilipitia jiji hilo lilipovamia Ukraine kupitia Belarus mnamo Februari 2022, kabla ya kuzuiwa na vikosi vya Kyiv.

Shambulio hilo lilijiri baada ya Putin kukutana na majenerali wakuu wa Urusi katika safari adimu ya kutembelea kituo  cha Rostov-on-Don kusini mwa Urusi.

Rais Zelensky alisema shambulio limeharibu pia chuo kikuu cha ufundi na ukumbi wa michezo. Baadhi ya majengo ya karibu pia yaliharibiwa kwenye shambulio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.