Pata taarifa kuu

Matamshi ya rais wa zamani wa Ufaransa kuhusu vita vya Ukraine yazua hisia

Nairobi – Rais wazamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy juma hili ameamsha hasira kutoka kwa utawala wa Kiev na Paris, baada ya kupendekeza kuwa uvamizi nchini Ukraine unaweza kumalizika ikiwa kutafanyika kura mpya ya maoni katika majimbo yanayokaliwa na Urusi.

Aidha ameitaka nchi ya Ukraine kubakia kutokuwa na upande na kwamba haina nafasi kwenye umoja wa Ulaya wala NATO
Aidha ameitaka nchi ya Ukraine kubakia kutokuwa na upande na kwamba haina nafasi kwenye umoja wa Ulaya wala NATO AFP - BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yake yaliyochapishwa juma hili na gazeti la Le Figaro, Sarkozy alisema raia wa Ukraine wangependa kurejesha maeneo yao waliyoporwa, lakini ikiwa watashindwa kufanya hivyo kupitia vita basi itabidi kufanyike kura ya maoni itakayosimamiwa na jumuiya ya kimataifa.

Akizungumzia hasa enei la Crimea ambalo lilitwaliwa na Urusi kwa nguvu mwaka 2014, rais huyo wazamani amesema kwa Kiev kuwaza kurejesha eneo hilo mikononi mwake ni sawa na ndoto za mchana.

Sarkozy kwenye mahojiano hayo aliongeza kuwa kinachofanywa na Urusi, hakimaanishi kuwa Vladmir Putin hakufikiria kabla ya kuchukua maamuzi aliyoyafanya, kauli ambayo imekashifiwa vikali na utawala wa Paris na Kiev.

Aidha ameitaka nchi ya Ukraine kubakia kutokuwa na upande na kwamba haina nafasi kwenye umoja wa Ulaya wala NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.