Watu 33 wamefariki katika mlipuko nchini Urusi
Nairobi – Takriban watu 33 wameuwa katika mlipuko kwenye kituo cha petroli katika jimbo linalojitawala la Dagestan nchini Urusi, wizara ya afya imethibitisha.
Imechapishwa:
Watu 80 wameripotiwa kujeruhiwa wakiwemo watoto watatu kwenye mlipuko huo katika mji wa Makhachkala. Rais Putin ametuma pole zake kwa waathirwa wa mkasa huo.
Picha zilizosambazwa na wizara ya masuala ya dharura nchini humo zimeonyesha magari yalioharibiwa vibaya katika mlipuko huo wakati maofisa wa uokozi wakijaribu kuzima moto mkubwa katika eneo la tukio.
Serikali imsema watu 30 walifariki katika mkasa huo wakati wengine 80 wakiwa wakiachwa na majeraha.
Mlipuko huo umetokea katika mji wa Makhachkala baada ya moto kutokea katika kituo kimoja cha petrol.
Mamlaka imesema mlipuko huo pia umeharibu majengo na magari mengine yaliokuwa karibu na eneo la tukio. Tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.
Serikali ya Dagestan imetangaza siku ya Agosti 15 kuwa siku ya maombolezo.