Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Urusi: Alexei Nalvalny ahukumiwa kifungo kipya cha miaka 19 jela

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny, 47, amehukumiwa Ijumaa hii, Agosti 4, 2023, kifungo kipya cha miaka 19. Wakati tayari amefungwa, atalazimika kutumikia kifungo hiki kipya katika jela lenye masharti magumu anakozuiliwa.

Alexeï Navalny alipowasili kusikiliza uamuzi wa kesi yake, katika jela ya IK-6, Ijumaa hii Agosti 4, 2023.
Alexeï Navalny alipowasili kusikiliza uamuzi wa kesi yake, katika jela ya IK-6, Ijumaa hii Agosti 4, 2023. AFP - ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Alexei Navalny amepatikana na hatia ya kuunda na kuongoza kundi lenye "msimamo mkali", ambalo ni shirika lake linalopambana dhidi ya ufisadi.

Waandishi wa habari hawakuweza kufikia chumba cha mahakama. Kesi hiyo ilishughulikia kwa dakika chache tu.

Msemaji wa kiongozi huyowa upinzani, Kira Iarmych, ndiye ambaye ametangaza uamuzi huo wa mahakama kwanza. "Alexeï Navalny atatumikia kifungo cha miaka 19, " amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani ukiitwa Twitter).

Kwa utawala maalum, lazima tuelewe kwamba mtu anayehusika sasa atawekwa kizuizini katika mojawapo ya vituo vikali zaidi katika mfumo wa magereza wa Kirusi (tazama sanduku).

Bw. Navalny amejibu, kwenye kituo chake cha Telegram na kwenye Facebook, akitoa wito kwa Warusi kuendelea "kupambana", licha ya kile anachoelezea kuwa "hukumu ya maisha".

"Ninajua kuwa, kama wafungwa wote wa kisiasa, ninatumikia kifungo cha maisha. Iwe tunazungumza juu ya maisha yangu, au ya serikali hii, "ameandika Bw. Navalny.

"Hukumu hii ya kinyama ni jibu la ujasiri wake wa kukosoa utawala wa Kremlin," amesema Michel. "EU inalaani vikali (...) kukamatwa kwake kwa sababu ya kisiasa, kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa. "

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Ujerumani, Annalena Baerbock, ameshutumu "kukosekana kwa haki".

"Putin haogopi chochote zaidi ya wale wanaopinga vita, ufisadi na kutetea demokrasia, hata kutoka kwa jela. Hatanyamazisha sauti muhimu, "amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Ujerumani.

"Kwa mara nyingine tena tunatoa wito kwa mamlaka ya Urusi kumwachilia Bw. Navalny mara moja na bila masharti, pamoja na wafungwa wote wa kisiasa", msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa amesema.

Washington "inalaani hukumu mpya ya mahakama" iliyotolewa kwa mpinzani wa Kirusi, kulingana na "mashtaka yasiyo ya msingi ya kile kinachoitwa "msimamo mkali", msemaji Matthew Miller amebaini.

Hatimaye, Umoja wa Mataifa unatoa wito wa "kutolewa mara moja" kwa mshindi wa 2021 wa Tuzo ya Sakharov ya Bunge la Ulaya.

Hatia hii, alisema Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, katika taarifa kwa vyombo vya habari, "inaibua wasiwasi mpya kuhusu unyanyasaji wa mahakama na utumiaji wa mfumo wa mahakama kwa madhumuni ya kisiasa nchini Urusi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.