Pata taarifa kuu

Washukiwa wa shambulio la kigaidi jijini Brussels wakutwa na hatia

Nairobi – Mahakama jijini Brussels nchini Ubelgiji, imewapata na hatia raia wa Ufaransa Salah Abdeslam na Mohamed Abrini mzaliwa wa nchi hiyo mwenye asili ya Morocco kuhusika na mashambulio ya bomu yaliyofanyika mwaka 2016 na kusababisha vifo vya watu 32.

Mahakama imewapata na hatia raia wa Ufaransa Salah Abdeslam na Mohamed Abrini mzaliwa wa nchi hiyo mwenye asili ya Morocco kuhusika na mashambulio ya bomu nchini Ubelgiji
Mahakama imewapata na hatia raia wa Ufaransa Salah Abdeslam na Mohamed Abrini mzaliwa wa nchi hiyo mwenye asili ya Morocco kuhusika na mashambulio ya bomu nchini Ubelgiji via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao tayari walikuwa wamepata kifungo cha maisha na Mahakama ya Ufaransa, baada ya kupatikana na kosa la kutekeleza mauaji ya watu 130 jijini Paris mwaka 2015.

Kesi hiyo imefikia ukingoni baada ya miaka kadhaa ya kusikilizwa ambapo wawili hao walikamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kutekeleza shambulio kwenye uwanja mkuu wa ndege jijini Brussels na kituo cha mabasi, mashambulio ambayo kundi la Islamic State lilidai kuhusika.

Watu waliojeruhiwa katika mashambulio hayo, walitumia miezi kadhaa kutoa ushahidi wao mbele ya Mahakama, wakiomba haki itendeke.

Baada ya Salah Abdeslam na Mohamed kupatikana na hatia, Mahakama inatarajiwa kuwahukumu maisha jela, mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.