Pata taarifa kuu

Odessa yakumbwa na mashambulizi, bei ya nafaka yanza kupanda tena

Makubaliano ya nafaka ambayo yaliruhusu nafaka ya Ukraine na mbolea ya Urusi kupita katika Bahari Nyeusi yalimalizika muda wake wa siku moja. Na asubuhi ya leo, makombora yalirushwa kwenye bandari ya Odessa, ripoti za Kyiv. Urusi imeendele kukosolea tangu kuchukua umauzi wa kusitishwa kwa mkataba wa nafaka ambao ulimalizika Jumatatu jioni , na bei ya nafaka inaongezeka.

"Operesheni za kupambana na ulinzi wa anga zinaendelea," Sergiy Bratchuk, afisa wa utawala wa mkoa wa Odessa, amesema kwenye Telegram.
"Operesheni za kupambana na ulinzi wa anga zinaendelea," Sergiy Bratchuk, afisa wa utawala wa mkoa wa Odessa, amesema kwenye Telegram. © Anastasia Becchio/RFI
Matangazo ya kibiashara

Awali Kvyiv ilitangaza kwamba ulinzi wa anga wa Ukraine umeimarishwa mapema siku ya Jumanne katika eneo la kusini la Odessa, eneo muhimu kwa mkataba wa nafaka ambao ulimalizika Jumatatu jioni, mamlaka nchini Ukraine imesema. "Operesheni za kupambana na ulinzi wa anga zinaendelea," Sergiy Bratchuk, afisa wa utawala wa mkoa wa Odessa, amesema kwenye Telegram.

Kulingana na makao makuu ya jeshi la Ukraine kusini mwa nchi, "adui anashambulia mikoa ya kusini na ndege zisizo na rubani", amesema kwenye Telegram.

Mashambulizi katika miji kadhaa nchini

Eneo la Kusini mwa Ukraine linalengwa na "mashambulizi ya ndege zisizo na rubani", gavana wa eneo hilo Oleg Kiper amebaini kwenye mtandao huo wa kijamii, akitoa wito kwa watu kusalia majumbani hadi tahadhari itakapoondolewa.

Arifa nyingi za uvamizi wa anga zmekuwa zikiendelea mapema Jumanne kote nchini, katika mikoa ya Odessa, Mykolaiv, Kherson, Zaporizhia lakini pia katika mikoa ya Donetsk (kusini-mashariki), Kharkiv (mashariki), Dnipropetrovsk (katikati-mashariki), Poltava (mashariki) , Kirovograd (katikati) na Cherkassy (katikati).

Odessa, ambayo mnamo Januari kituo chake cha kihistoria kiliandikwa kwenye orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia, imeshambuliwa kwa mabomu mara kadhaa tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, 2022.

Baada ya uvamizi wa Moscow kuanza, bandari za Bahari Nyeusi za Ukraine zilizuiliwa na meli za kivita za Urusi hadi makubaliano, yaliyotiwa saini mnamo Julai 2022 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa na Uturuki, ambayo yaliruhusu kupitisha usafirishaji wa nafaka muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.