Pata taarifa kuu

Moscow yataka kupanua mpango wa nafaka kwa siku 60 tu, Kyiv yakosoa masharti

Urusi imependekeza kupanua mpango wa uuzaji wa nafaka wa Ukraine, ambao unamalizika mnamo Machi 18, lakini kwa siku 60 tu na sio 120 kama ilivyokuwa hadi sasa. Ofa hiyo imekosolewa na Kyiv, ambayo inaiona kama swali la makubaliano ya awali limekiukwa, lakini hakuikataa rasmi.

Meli za mizigo zinazobeba nafaka zikisubiri ukaguzi chini ya makubaliano yaliyofikiwa chini ya mwafaka wa Umoja wa Mataifa na Uturuki, kati ya Urusi na Ukraine, hapa ilikuwa Bosphorus, mjini Istanbul, Desemba 11, 2022.
Meli za mizigo zinazobeba nafaka zikisubiri ukaguzi chini ya makubaliano yaliyofikiwa chini ya mwafaka wa Umoja wa Mataifa na Uturuki, kati ya Urusi na Ukraine, hapa ilikuwa Bosphorus, mjini Istanbul, Desemba 11, 2022. © Yoruk Isik / Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Verchinin amesema baada ya mazungumzo huko Geneva na maafisa wa Umoja wa Mataifa kwamba Moscow "haipingi kuongezwa tena kwa 'Mpango wa Bahari Nyeusi' baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo Machi 18, lakini kwa siku 60 pekee.

"Msimamo wetu wa siku za usoni utaamuliwa na maendeleo yanayoonekana katika kurekebisha mauzo yetu ya nje ya kilimo, sio kwa maneno, lakini kwa vitendo. Hii ni pamoja na malipo ya benki, vifaa vya usafirishaji, bima, 'kuzuiwa' kwa shughuli za kifedha na usambazaji wa amonia kupitia bomba la "Togliatti-Odessa", afisa huyo wa Urusi amesema.

Lakini Kyiv imekosoa masharti haya mapya. "Mkataba wa 'Black Sea Grain Initiative' unahusisha angalau siku 120 za kuongeza muda, msimamo wa Urusi wa kuurefusha kwa siku 60 pekee kwa hiyo unakinzana na waraka uliotiwa saini na Uturuki pamoja na Umoja wa Mataifa," amesema Waziri wa Miundombinu wa Ukraine Oleksandre Kubrakov,  akibainisha kuwa Kiev ilikuwa inasubiri "nafasi rasmi" ya Umoja wa Mataifa na Ankara, kama "wadhamini wa mpango huo".

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alihakikisha kwamba "Umoja wa Mataifa bado unashiriki kikamilifu katika Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi na kujitahidi kuwezesha usafirishaji wa mbolea na vyakula vya Urusi".

Muda mfupi baadaye, Umoja wa Mataifa ulisema katika taarifa kutoka Geneva (Uswisi) kwamba "unazingatia" pendekezo la Urusi na kusisitiza kwamba mkuu wa Umoja wa Mataifa "amethibitisha kwamba Umoja wa Mataifa utafanya kila linalowezekana ili kuhifadhi uadilifu wa Mpango wa Nafaka [. ..] na kuhakikisha kuendelea kwake".

Mjini Geneva, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Verchinin alisema alikuwa na mazungumzo "ya uwazi na ya kina" na mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths na katibu mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (Unctad), Rebeca Grynspan.

Mazungumzo haya, alisema, yalitumika "kuthibitisha tena kwamba wakati mauzo ya kibiashara ya bidhaa za Ukraine yanafanyika kwa kasi ya kutosha na kuleta faida kubwa kwa Kyiv, vikwazo vilivyowekwa kwa wasafirishaji wa kilimo wa Urusi bado viko ".

China ni nchi ya kwanza kupokea

Mkataba huu wa "Bahari Nyeusi", uliotiwa saini mwezi Julai 2022 kwa siku 120 kati ya Umoja wa Mataifa, Ukraine, Urusi na Uturuki, ulikuwa na matokeo ya kupunguza mzozo wa chakula duniani uliosababishwa na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24, 2022. Ulifanywa upya mwezi Novemba kwa muda wa miezi minne na kuruhusiwa mauzo ya nje ya zaidi ya tani milioni 24 za nafaka kutoka bandari za Ukrainei, kulingana na Umoja wa Mataifa.

China ndiyo mpokeaji mkuu wa mauzo ya nje chini ya mpango huo, ikifuatiwa na Uhispania na Uturuki, ambayo inashika nafasi ya tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.