Pata taarifa kuu

Watu sita wauawa katika shambulio la anga la Urusi mashariki mwa Ukraine

Gavana wa Ukraine Pavlo Kyrylenko ametangaza kuwa shambulio la anga la Urusi mashariki mwa Ukraine siku ya Jumamosi limeua watu sita katika siku ya 500 ya vita.

Katika picha hii iliyotolewa na Idara ya huduma ya dharura ya Ukraine, maafisa wa idara ya huduma za dharura wanafanya kazi katika eneo la shambulio la anga la Urusi, huko Lyman, mkoa wa Donetsk, Ukraine, Jumamosi, Julai 8, 2023.
Katika picha hii iliyotolewa na Idara ya huduma ya dharura ya Ukraine, maafisa wa idara ya huduma za dharura wanafanya kazi katika eneo la shambulio la anga la Urusi, huko Lyman, mkoa wa Donetsk, Ukraine, Jumamosi, Julai 8, 2023. © Ukrainian Emergency Service / AP
Matangazo ya kibiashara

"Takriban watu sita waliuawa na watano kujeruhiwa" katika shambulio hili la anga katika mji wa Lyman, amesema gavana wa mkoa wa Donetsk kwenye mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo Volodymyr Zelensky amechapisha video yake akitembelea kisiwa ambacho kilikuja kuwa ishara ya upinzani wa Ukraine, wakati vita vinaingia siku yake ya 500.

Mwanzoni mwa vita, askari wa Ukraine wanaotetea Kisiwa cha Nyoka walikaidi amri kutoka kwa meli ya kivita ya Urusi ya kujisalimisha.

Kisiwa hicho kilichopo kwenye Bahari Nyeusi kilitekwa na Urusi lakini baadaye kikarudishwa na Ukraine.

Katika video, rais wa Ukraine amekiita kisiwa hiki "mahali pa ushindi" ambapo hakitaweza kutekwa tena.

Zaidi ya watoto 500 wauawa tangu vita vilipoanza 

Hayo yanajiri wakati Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watoto 500 walikufa katika siku 500 za vita nchini Ukraine.

Zaidi ya watoto 500 walikufa katika siku 500 za vita, kulingana na Umoja wa Mataifa, idadi ya jumla ya raia nchini Ukraine ambao wamekufa tangu mwanzo wa vita, tangu Februari 24, 2022, imepita watu elfu 9, data ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa iliripoti siku moja kabla.

Kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine, watoto 494 wanaripotiwa kuwa ndio ambao wameuawa hadi sasa, na zaidi ya watoto 1,050 walijeruhiwa.

Watoto wengi waliteseka katika mikoa ya Donetsk, Kharkiv, Kyiv, Kherson, Zaporozhye, Mykolaiv, Dnepropetrovsk, Chernihiv na Lugansk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.