Pata taarifa kuu

Watalaam wa nyukilia kuzuru Zaporizhzhia Kusini mwa Ukraine

Nairobi – Shirika la Umoja wa Mataifa, Shirika la umoja wa mataifa linalothathmini matumizi ya nishati ya Atomic inataka kuruhusiwa kwenda kuangalia hali ya kituo cha  nyuklia cha Zaporizhzhia Kusini mwa Ukraine, wakati huu Kiev na Moscow zikilaumiana kuhusu uvamizi katika kiwanda hicho kikubwa cha barani Ulaya.

Ukraine na Urusi zimekuwa zikithumiana kuhusu uwepo wa njama za kulipua kinu hicho cha nyukilia
Ukraine na Urusi zimekuwa zikithumiana kuhusu uwepo wa njama za kulipua kinu hicho cha nyukilia REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Rafael Grossi amesema watalaam wake wanahitaji muda zaidi wa kwenda kuthathmini uwepo wa vilipuzi katika kituo hicho cha nyuklia.

Ameongeza kuwa hii ni muhimu kutokana na mwendelezo wa wasiwasi wa kijeshi kati ya Ukraine na Urusi katika eneo hilo.

Hata hivyo, watalaam wa shirika hilo walizuru  kituo hicho cha Zaporizhzhia lakini hawakubaini vilipuzi vyovyote, lakini kutokana na kuendelea kwa mapigano, kuna wasiwasi.

Wito huu wa Shirika hilo umekuja wakati huu Ukraine na Urusi, zikilaumiana kuhusu kuwepo kwa mpango wa kushambulia kituo hicho, lakini hakuna ushahidi wa madai hayo kutoka pande hizi mbili.

Baada ya kuivamia Ukraine mwezi Februari mwaka uliopita, wanajeshi wa Urusi wameendelea kudhibiti eneo la Zaporizhzhia tangu mwezi Machi mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.