Pata taarifa kuu

Moscow yadai tangazo la Marekani kutuma silaha tata kwa Ukraine, ni 'kitendo cha udhaifu'

Urusi imechukulia tangazo la kutuma mabomu ya cluster kwa Ukraine, uamuzi uliochukuliwa na Marekani ni "kitendo cha udhaifu" ambacho kitaifanya Washington "kushiriki" katika vifo vya raia vilivyosababishwa na silaha hii yenye utata.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ahudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa njia ya video kwenye Ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Julai 4, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ahudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) kwa njia ya video kwenye Ikulu ya Kremlin huko Moscow mnamo Julai 4, 2023. AFP - ALEXANDER KAZAKOV
Matangazo ya kibiashara

"Kutumwa kwa mabomu ya cluster ni ishara ya kukata tamaa na kukubali udhaifu katika muktadha wa kushindwa kwa kile kinachojulikana kama mashambulizi ya Ukraine," Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa.

Kwa upande mwingine rais wa Marekani Joe Biden ametetea "uamuzi wake wa kuipa Ukraine mabomu ya cluster, ambayo yana rekodi ya kuua raia.

Rais alisema ilimchukua "muda kushawishika kufanya hivyo", lakini alichukua hatua kwa sababu "Waukraine wanaishiwa na risasi".

Kiongozi wa Ukraine alipongeza hatua hiyo "iliyofaa", lakini mashirika ya haki za binadamu na baadhi ya wajumbe kutoka chama cha Democratic walikosoa uamuzi huo.

Mshauri wa usalama wa kitaifa Jake Sullivan alisema kwamba "wanatambua mabomu ya hayo yanaleta  madhara kwa raia" kutokana na mabomu ambayo hayajalipuka.

"Hii ndiyo sababu tumeahirisha uamuzi huo kwa muda mrefu tuwezavyo."

Sullivan alisema Ukraine inaishiwa na silaha na ilihitaji kupigwa jeki huku Marekani ikiongeza uzalishaji  wake wa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.