Pata taarifa kuu

Zelensky aishukuru Washington kwa misaada yake ya ulinzi "ya lazima" kwa Ukraine

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemshukuru mwenzake wa Marekani Joe Biden siku ya Ijumaa kwa msaada wa kijeshi 'muhimu' kwa ulinzi wa Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, huko Kyiv, Ukraine, Julai 1, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, huko Kyiv, Ukraine, Julai 1, 2023. © Sergei CHUZAVKOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Msaada wa kijeshi wa lazima, mpana na wa wakati unaofaa," Volodymyr Zelensky almeandika kwenye mitandao ya kijamii, akimshukuru Joe Biden na Wamarekani kwa "hatua hizi madhubuti." "Kuongeza uwezo wa ulinzi wa Ukraine kutaleta zana mpya za kukomboa eneo letu na kutuleta karibu na amani," ameongeza.

Kwa hakika, silaha hizi hutawanya milipuko midogo midogo bila mpangilio katika maeneo yenye upana wa viwanja vinne vya soka. Baadhi ya mabomu hayalipuki na kwa hivyo huwa hatari kwa miongo kadhaa baada ya mzozo.

Kwa kawaida sheria ya Marekani inakataza uzalishaji na usafirishaji wa zilaha hizi zenye kiwango cha kutofaulu zaidi ya 1%, ambacho kinashughulikia karibu ghala zote za Marekani. Lakini Joe Biden anakusudia kukwepa kikwazo hiki kwa kutegemea kanuni nyingine: anaweza kutoa msaada wowote wa kijeshi ikiwa ataona kuwa ni kwa maslahi ya usalama wa taifa wa nchi yake.

Alipoulizwa kuhusu suala hili la mabomu na silaha nzito, Katibu Mkuu wa NATO amekumbusha Ijumaa kwamba haya yalikuwa maamuzi ya serikali yeyewe, bila ya shirika, anasema mwandishi wetu wa Brussels, Jean-Jacques Hery. Na Jens Stoltenberg kukumbusha kwamba katika mgogoro huu, silaha hizi hutumiwa na Ukraine na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.