Pata taarifa kuu

Ramaphosa: Ziara yetu nchini Ukraine na Urusi ilikuwa ya mafanikio

NAIROBI – Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amesema ziara ya viongozi wa Afrika nchini Ukraine na Urusi kujaribu kuleta amani ili vita vinavyoendelea vikome, imekuwa ya kihistoria na mafanikio.

Viongozi wa Afrika wamikutana na rais wa Urusi na mwenzake wa Ukraine
Viongozi wa Afrika wamikutana na rais wa Urusi na mwenzake wa Ukraine AP
Matangazo ya kibiashara

Ramaphosa, ametoa kauli hiyo, baada ya kukutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky jijini Kiev na Vladimir Putin jijini Saint Petersburg na kuwasilisha mapendekezo ya kusitisha vita.

Hata hivyo, haijafahamika iwapo ziara hiyo imeleta matokeo chanya.

Ramaphosa ambaye aliambatana na marais kutoka Senegal, Zambia, na Comoro amesema ziara yao, ilipaza sauti ya bara la Afrika kuhusu vita hivyo ambavyo vimesababisha kupanda kwa gharama ya maisha hasa kwa waafrika.

Wakati wa ziara hiyo, Ramaphosa amesema ujumbe huo uliwasilisha mapendekezo 10 ikiwemo kuacha vita na kila nchi kuheshimu mipaka ya nchi nyingine, lakini Urusi imesema mapendekezo hayo ni magumu kutekeleza, huku Ukraine ikisema haiwezi kuingia kwenye mazungumzo na Urusi hadi pale itakapowaondoa wanajeshi wake katika ardhi yake.

Ujumbe kutoka Afrika, unatumai kuwa pande hizo mbili zinaweza kutumia mapendekezo hayo, kuanza mchakato wa kusitisha vita, lakini inavyoonekana kila upande unamaamini kuwa utashinda vita hivyo kwa kuendelea kupambana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.