Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Marekani itaipatia Kyiv silaha nzito zenye utata

Marekani itatoa silaha na mabomu  kwa Ukraine, Ikulu ya Marekani imesema siku ya Ijumaa, Julai 7, ikivuka kizingiti muhimu katika aina ya silaha zinazotolewa kwa Kiev ili kujilinda dhidi ya Urusi. Silaha hizi zimepigwa marufuku na zaidi ya nchi 120 kwa sababu ya athari mbaya kwa raia. Kwa hiyo uamuzi huo una utata. Unakuja wakati washirika wana wasiwasi juu ya kujikokota kwa mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Urusi.

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan akihutubia suala la kuipa silaha nyingi Ukraine wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila siku katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Julai 7, 2023.
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan akihutubia suala la kuipa silaha nyingi Ukraine wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila siku katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Julai 7, 2023. © Jonathan Ernst / Reuters
Matangazo ya kibiashara

“Ni uamuzi mgumu. Tulichelewesha" kwa muda, mshauri wa usalama wa kitaifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan amewaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa "ni jambo sahihi kufanya". Amebaini kwamba Rais Joe Biden alifanya uamuzi huo kwa kushauriana na washirika na baada ya "pendekezo la kauli moja" kutoka kwa utawala wake.

Inavyoonekana, majadiliano yalikuwa makali ndani ya utawala wa Biden. Je, tukubali au tusikubali mahitaji ya Ukraine yanayozidi kuwa ya dharura ya kusambaza aina hii ya silaha ambayo zaidi ya nusu ya nchi duniani zimepiga marufuku? Kulingana na Gazeti la Washington Post, kulikuwa na wasiwasi juu ya mashambulizi ya Ukraine.

Silaha hizi zitatumiwa na na silaha zingine nzito za howitzer ambazo Marekani tayari iliipa Ukraine. Washington, kama Moscow au Kyiv, haijatia saini mkataba wa kimataifa ambao unakataza matumizi ya silaha hizi hatari kwa raia. Jake Sullivan, hata hivyo, amehakikisha kwamba Ukraine ilitoa dhamana "iliyoandikwa" juu ya matumizi itakayotengeneza silaha hizi ili kupunguza "hatari inayoweza kutokea  kwa raia".

'Msaada wa lazima'

Tangazo hilo linakuja kama sehemu ya mpango mpya wa msaada wa kijeshi wa dola milioni 800 kwa Ukraine ambao utaleta jumla ya usaidizi wa kijeshi wa Marekani tangu vita kuanza mwezi Februari 2022 hadi zaidi ya dola bilioni 41. Mbali na silaha hizi, Marekani itatoa magari ya kivita, silaha za nzito za kivita, silaha za kukinga vifaru na vifaa vingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.