Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-USHIRIKIANO

Rais wa Ukraine Zelensky kuzuru Bulgaria

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzuru Bulgaria leo. Ziara hii inafanywa kwa siri, lakini kwa maoni ya wataalam, inahusu kuipa silaha Ukraine. Mazingira ya kisiasa yanaendelea kugawanyika kuhusiana na vita vya Ukraine na mtazamo wa unaopaswa kutumiwa kwa Kiev na Moscow.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa kikao cha Bunge la Ukraine, mjini Kyiv, Jumatano, Juni 28, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wakati wa kikao cha Bunge la Ukraine, mjini Kyiv, Jumatano, Juni 28, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Sofia, Damian Vodenitcharov

Ziara hii inafanyika kuwa siri. Au angalau haijathibitishwa na taasisi yoyote ya umma. Waziri wa Ulinzi tu Todor Tagarev amekiri katika mahojiano ya televisheni kwamba ni zaiara ambayo iliandaliwa tangu mapema.

Ziara za kigeni za Volodymyr Zelensky kawaida hufanyika kwa siri kwa sababu za usalama. Muungano unaotawala kati ya vyama vya mawaziri wakuu wa zamani Boyko Borissov na Kiril Petkov ulikaribisha ziara ya Zelensky. Chama cha ultra-nationalist na kinachounga mkono Urusi Renaissance kimetangaza kuwa rais wa Ukraine hatakaribishwa nchini Bulgaria. Chama cha Kisoshalisti, ambacho pia kinaunga mkono Urusi, kimeonyesha upinzani wake wa kupeleka silaha kwa Ukraine, ambacho kimesema kilitaka kumwambia Zelensky mwenyewe.

Mnamo 2022, Bunge la Bulgaria lilikataa kumpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba au kusikia ujumbe kutoka kwa Volodymyr Zelensky. Serikali mpya iliyochaguliwa hata hivyo imetangaza nia yake ya kutuma silaha moja kwa moja kwa Ukraine, lakini sio ndege za kivita za MIG-29 au vifaru, vinavyotamaniwa sana na wanajeshi wa Ukraine. Kuuzwa tena kwa vinu vya nyuklia vilivyotengenezwa na Urusi vilivyonunuliwa na Bulgaria lakini ambavyo havijatumika pia vinaweza kuwa sehemu ya majadiliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.