Pata taarifa kuu

Ukraine: Operesheni za jeshi dhidi ya Urusi, imeendelea kwa kasi ndogo: Zelensky

NAIROBI – Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky, amenukuliwa hapo jana akisema operesheni za majeshi yake dhidi ya Urusi, imeendelea kwa kasi ndogo kuliko alivyotarajia, lakini akasisitiza hawana haja ya kuharakisha mkakati wao.

Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky, amenukuliwa hapo jana akisema operesheni za majeshi yake dhidi ya Urusi, imeendelea kwa kasi ndogo
Rais wa Ukraine, Volodymry Zelensky, amenukuliwa hapo jana akisema operesheni za majeshi yake dhidi ya Urusi, imeendelea kwa kasi ndogo © zelensky
Matangazo ya kibiashara

Rais Zelensky alinukuliwa na shirika la habari la Uingereza, ambapo alikiri mapigano kuwa makali katika maeneo wanayojaribu kuchukua, hata hivyo akisisitiza kuwa pamoja na kasi ndogo, wamefanikiwa kuchukua maeneo kadhaa.

Aidha katika hotuba yake kwa viongozi wa Ulaya nan chi wafadhili, rais Zelensky, amesisitiza umuhimu wan chi yake kuendelea kusaidiwa kwa zana za kijeshi ili kukabili vilivyo mashambulio ya Urusi, huku akionesha ni kwanini nchi za ukanda lazima zikae macho na vitendo vya Urusi.

Hata hivyo matamshi yake yamepingwa vikali na rais wa Urusi, Vladmir Putin, ambaye kwa upande wake amejinasibu vikosi vyake kudhibiti operesheni za wanajeshi wa Kiev, na kwamba Ukraine imepoteza wanajeshi wengi.

Mwanzoni mwa juma hili, Kiev ilitangaza kufanikiwa kuchukua vijiji zaidi ya 8 kusini mwa nchi hiyo na kuzunguka eneo la Zaporizia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.