Pata taarifa kuu

Ukraine: Mvutano waripotiwa kati Rais Zelensky na Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko

Kulingana na vyanzo kadhaa, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky angependa kumfuta kazi Vitali Klitschko kwenye nafasi ya uongozi wa utawala wa serikali ya jiji la Kiev, akimtuhumu bondia huyo wa zamani kwa usimamizi mbaya wa mahandaki ya chini ya ardhi wakati wa uvamizi wa Urusi. Mvutano wa kiiasa nchini Ukraine ulikuwa umetulia kwa kiasi fulani tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi.

Meya wa Kyiv Vitali Klitschko akiwa katika mahandaki ya chini ya ardhi wakati wa uvamizi mnamo Juni 1, 2023.
Meya wa Kyiv Vitali Klitschko akiwa katika mahandaki ya chini ya ardhi wakati wa uvamizi mnamo Juni 1, 2023. REUTERS - VALENTYN OGIRENKO
Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Kyiv,

Yote yalianza Juni 1, 2023. Siku hiyo, kombora la Urusi lilipiga viunga vya mashariki mwa Kiev, na kuua wanawake wawili na mtoto mmoja ambao hawakuweza kufikia makazi ya chini ya ardhi ya karibu kwa sababu yalikuwa ymefungwa kwa ufunguo. Tukio lililozua hasira kwa wakaazi wa mji wa Kiev, na Volodymyr Zelensky mara moja aliwashambulia "maadui wa ndani", akishutumu utawala wa jiji la Kyiv kwa uzembe katika usimamizi wa makazi ya uvamizi wa anga.

Bila kumtaja jina, Volodymyr Zelensky alimshambulia maneno Vitali Klitschko, akisema "kuna hali ya kutoaminiana" kati yake na mkuu utawala wa serikali ya jiji la Kiev. Klitschko wakati huo huo alishutumu "kampeni iliyofunguliwa", akishutumu ofisi ya rais kwa kutaka kuchukuwa udhibiti wa manispaa ya jiji Kyiv.

Kwa kweli, mzozo kati ya watu hao wawili sio mpya. Mnamo mwaka wa 2019, Chama cha Zelensky, Mtumishi wa raia, kilijaribu bila mafanikio kuchukua udhibiti wa manispaa ya jiji la mji wa Kiev kutoka kwa Klitschko, mshirika wa muda mrefu wa Rais wa zamani Petro Poroshenko. Bila mafanikio, bondia huyo wa zamani alishinda uchaguzi, wakati chama cha Zelensky hakikufanikiwa kabla ya vita kuwaweka wagombea wake katika miji mikubwa ya Ukraine, ya Dnipro, Odessa au Kharkiv.

Kuzingirwa kwa Kyiv na jeshi la Urusi mnamo mwezi Machi 2022 kulizima uhusiano mbaya kati ya Zelensky na Klitschko. Hata hivyo, uhusiano huo mbaya uko katika mchakato wa kuanzishwa upya, huku utawala wa rais ukipenda kurudisha usimamizi wa masuala ya mji mkuu katika kambi yake.

Hata hivyo, ni ukweli kwamba Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake wanaona Klitschko kama mpinzani anayewezekana katika siku zijazo, wanamwogopa sana. Kura za maoni hazidanganyi: kiwango cha kuidhinishwa kwa hatua ya Volodymyr Zelensky katika jamii ni 83%, dhidi ya 48% ya Vitali Klitschko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.