Pata taarifa kuu

Urusi: Lengo la uasi lilikuwa kuokoa Wagner, sio 'kupindua serikali', anasema Prigozhin

Mkuu wa kundi la wanamgambo la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amesema Jumatatu Juni 26 katika ujumbe wa kwanza wa sauti baada ya kumalizika kwa uasi wake kwamba lengo lake haikuwa kupindua serikali ya Urusi, bali kuokoa kundi lake la kijeshi lililokuwa likitishiwa kuangamizwa na jeshi.

Mkuu wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, huko Rostov-sur-le-Don, katika video iliyorushwa hewani mnamo Juni 24, 2023 kwenye Telegram.
Mkuu wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, huko Rostov-sur-le-Don, katika video iliyorushwa hewani mnamo Juni 24, 2023 kwenye Telegram. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Ni hotuba ya kwanza ya mkuu wa kundi la wanamgambo la Wagner tangu kusitishwa kwa uasi  ambao ulifanya Moscow kuwa na wasiwasi mkubwa. Katika ujumbe wa daikika 11, kiongozi wa kundi hilo la mamluki amesema kwamba "lengo la uasi wao haikuwa kuwezesha uharibifu dhidi ya kundi la Wagner". Pia amehakikisha kwamba lengo halikuwa "kubadili serikali nchini".

Kwa upande mwingine, kulingana na Yevgeny Prigozhin, kusonga mbele kwa Wagner kuelekea katika mji mkuu wa Urusi, Moscow, wakati wa uasi wake Jumamosi ulibainisha "shida kubwa za usalama" nchini Urusi. Yevgeny Prigozhin anadai kwamba wapiganaji wake wamesafiri km 780huku wakikabiliana na upinzani mdogo. "Tulizuia vitengo vyote vya jeshi na tuliweza kudhibiti viwanja vidogo vidogo vya ndege tulipokuwa tukielekea Moscow ndani ya kipindi cha saa 24, tulisafiri umbali ambao askari wa Urusi walisafiri mnamo Februari 24, 2022 (siku ya mwanzo wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine). 

Amebaini kwamba, wakiwa njiani, wapiganaji wake walipokea msaada wa wakaazi wa maeneo walikopita wakati wa uasi wake nchini Urusi. "Raia walikuja kutulaki na kutupongeza wakiwa wameshikilia bendera za Urusi na nembo za Wagner, walifurahi tulipofika na tulipita karibu nao," amesema.

Mkuu wa kundi la Wagner pia alibaini kwamba Wagner walidondosha ndege za Jeshi la Anga la Urusi, madai ambayo Moscow haikuthibitisha. "Tunasikitika kwa kuziangusha baadhi ya nege za Urusie, lakini tulilazimika kufanya hivyokwani ndee hizo zilikuwa zikiturushia mabomu na makombora," amesema.

Yevgeny Prigozhin pia amesema kwamba rais wa Belarus Alexandre Loukachenko, ambaye alihudumu Jumamosi 24 Juni kama mpatanishi kati ya Kremlin na Wagner, alipendekeza suluhisho za kuwezesha kundi la wanamgamo la Wagner kuendelea kufanya kazi. Katika ujumbe huu, mkuu wa Wagner hakuonyesha ni wapi yupo, wakati Kremlin ilihakikisha kwamba ataondoka kwenda uhamioshoni nchini Belarus, bila kusema lini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.