Pata taarifa kuu

Urusi: Uasi ulioshindwa wa Prigozhin wasababisha madhara makubwa ya miundombinu

Takriban nyumba kumi na tano na zaidi ya 10,000 m2 za barabara ziliharibiwa wakati wa uasi wa silaha wa kundi la Wagner nchini Urusi, viongozi nchii humo walitangaza Jumapili Juni 25, wakitoa ripoti ya kwanza ya matukio haya ambayo yalitikisa utawala wa Urusi.

Watu wakikusanyika barabarani huku wapiganaji wa kundi la mamluki la kibinafsi la Wagner wakitumwa karibu na makao makuu ya jeshi katika moja ya wilaya ya kusini katika jiji la Rostov-on-Don, Urusi, Juni 24, 2023.
Watu wakikusanyika barabarani huku wapiganaji wa kundi la mamluki la kibinafsi la Wagner wakitumwa karibu na makao makuu ya jeshi katika moja ya wilaya ya kusini katika jiji la Rostov-on-Don, Urusi, Juni 24, 2023. © REUTERS / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kati ya Ijumaa jioni na Jumamosi jioni, kiongozi wa kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ambaye wapiganaji wake wanapigana nchini Ukraine, aliongoza uasi wa kustaajabisha wa silaha katika ardhi ya Urusi ambao ulilenga kupindua uongozi wa kijeshi ambao umekuwa katika vita vya wazi tangu miezi kadhaa.

Akiwa na wapiganaji wake, mfanyabiashara huyo alichukua udhibiti wa jiji la Rostov (kusini) na msafara wake ulivuka mikoa kadhaa, hadi kufikia umbali wa kilomita mia chache kutoka Moscow, na kusababisha mshangao nchini Urusi na ugenini.

Makabiliano karibu na Elizavetovka

Katika mkoa wa Voronezh, unaopakana na Ukraine na hatua ya maandamano haya ya yaliyoshindwa hadi mji mkuu wa Urusi, "nyumba 19 ziliharibiwa katika kijiji hiki", alisema Jumapili kwenye Telegram mkuu wa wilaya ya Pavlovsky.

Uharibifu huu ulifanyika "kufuatia makabliano ambayo yalitokea karibu na Elizavetovka, katika wilaya ya Pavlovsky, Juni 24, wakati safu ya kundi la Wagner ilivuka mkoa wetu", alisahihisha.

Kwa hivyo afisa wa eneo hilo alithibitisha kwamba msafara wa wapiganaji wa Wagner ulipambana katika eneo hilo na jeshi la serikali, bila kutoa maelezo zaidi juu ya uhasama huo.

Wala Wagner wala jeshi la Urusi katika hatua hii hawajazungumza rasmi juu ya waathiriwa wanaohusishwa na mapigano haya.

Zaidi ya 10,000 m2 ya barbara yaharibika

Huko Rostov, ambapo kundi la Wagner lilichukua makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji siku ya Jumamosi, "zaidi ya 10,000 m2 ya barabara ya lami" iliharibiwa, kulingana na meya, Alekseï Logvinenko.

Katika picha alizochapisha kwenye kituo chake cha Telegram, kunaonekana barabara zilizoharibiwa na vifaru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.