Pata taarifa kuu

Bwawa la Kakhovka: Macron atangaza kutuma 'msaada' kutokana na "mahitaji ya haraka" ya Ukraine

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumatano kutumwa, "saa zijazo sana", "msaada wa kukidhi mahitaji ya haraka" ya Ukraine katika uso wa uharibifu wa bwawa la umeme la Kakhovka kusini mwa nchi hiyo.

Kwenye picha hii kunaonekana eneo lililokumbwa na mafuriko baada ya bwawa la Nova Kakhovka kuvunjika, wakati ambapo Urusi ilishambulia Ukraine, huko Kherson, Ukraine Juni 7, 2023.
Kwenye picha hii kunaonekana eneo lililokumbwa na mafuriko baada ya bwawa la Nova Kakhovka kuvunjika, wakati ambapo Urusi ilishambulia Ukraine, huko Kherson, Ukraine Juni 7, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Ufaransa inalaani kitendo hiki kiovu ambacho kinahatarisha raia," rais wa Ufaransa, amesema kwenye Twitter baada ya mahojiano ya simu na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky. 

"Niliweza kumwambia Rais Zelensky mshikamano wangu na raia wake baada ya shambulio kwenye bwawa la Kakhovka," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.