Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Berlin yafunga balozi nne za Urusi, Moscow yashutumu 'uchochezi'

Siku chache zilizopita, Moscow iliamua kwa upande mmoja kupunguza uwepo wa wanadiplomasia wa Ujerumani kwenye ardhi yake. Berlin inajibu, Jumatano, Mei 30.

Ubalozi wa Ujerumani huko Moscow utalazimika kuachisha kazi watu zaidi ya mia moja, kufuatia hatua ya Moscow kupunguza idadi ya balozi za Ujerumani nchini Urusi.le 27 mai 2023
Ubalozi wa Ujerumani huko Moscow utalazimika kuachisha kazi watu zaidi ya mia moja, kufuatia hatua ya Moscow kupunguza idadi ya balozi za Ujerumani nchini Urusi.le 27 mai 2023 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku chache baada ya kukabiliwa na hatua ya kupunguziwa idadi ya mabalozi wake nchini Urusi, Ujerumani imeamua kufanya vivyo hivyo kwa Moscow. Siku ya Jumatano Mei 31, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ametangaza kufunga balozi nne kati ya tano za Urusi zilizopo nchini humo. "Ili kuhakikisha usawa wa uwepo wa pande zote katika kiwango cha wafanyakazi na miundo, tumeamua kuondoa idhini ya kufanya kazi kwa balozi nne kati ya tano za Urusi zinazoendeshwa nchini Ujerumani, hii imewasilishwa leo kwenye Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi, ” Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani amesema katika mkutano na wanahabari.

Ubalozi mdogo wa tano tu na ubalozi wa Urusi huko Berlin ndio utaweza kuendelea kufanya kazi. Berlin pia iliamua kufunga balozi zake tatu nchini Urusi mnamo mwezi Novemba - Kaliningrad, Yekaterinburg na Novosibirsk.

Urusi imekashifu uamuzi wa Berlin na kushutumu "uchochezi" ambao hautapita bila jibu kutoka Moscow. "Berlin inapaswa kuwa na shaka kidogo kwamba vitendo hivi vya uchochezi visivyo na mawazo havitapita bila majibu yetu ya haki," Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema katika taarifa.

Tangazo hili la Ujerumani linafuatia uamuzi wa hivi majuzi wa mamlaka ya Urusi kupunguza kwa kiasi kikubwa, kufikia Juni, idadi hiyo ya mabalozui wa Ujerumani katika ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.