Pata taarifa kuu

Ujerumani ;Tutaipa Ukraine msaada wa kijeshi wa Euro bilioni 2.7

Nairobi – Nchini Ujerumani wizara ya ulinzi  imetangaza kuwa itapeleka msaada wa vifaa vya kijeshi nchini Ukraine vitakavyogharimu euro bilioni 2.7, (dola bilioni 2.97) ikiwa ni pamoja na Vifaru 30 vyenye lebo ya Leopard.

Vifaru na wanajeshi wa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine.
Vifaru na wanajeshi wa Urusi karibu na mpaka wa Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Kando na Vifaru hivyo nchi hiyo itatoa ndege 200 zisizo na rubani na zaidi ya magari 200 yatakayotumika kijeshi na kwa ajili ya usambazaji wa vifaa. Hii ni kulingana na taarifa aliyotoa Andriy Yermak kwenye mtandao wake wa Telegram.

Msaada huo unasemakana kuwa mkubwa zaidi kutolewa na nchi hiyo licha ya kua nchi zingine zimekua zikitoa msaada kwa nchi hiyo iliyovamiwa na Urusi.

Haya yakijiri vikosi vya Urusi  vinasemekana viliondoka katika mji wa Bakhmut siku nne zilizopita.

Ujerumani inaisaidia Ukraine kwa kusambaza silaha na vifaa kutoka kwa akiba yake ya Bundeswehr, na vile vile kutoka kwa usafirishaji wa sekta ya ulinzi ambao hulipwa kwa fedha kutoka kwa bajeti ya Serikali ya Ujerumani. Wakati wa kutoa msaada, Serikali ya Ujerumani hurekebisha misaada yake kulingana na mahitaji ya Ukraine na kuendelea kuchunguza ni wapi inaweza kuongeza usaidizi wake.

Ujerumani pia ni mchangiaji mkubwa zaidi wa hazina ya ufadhili wa Mfuko wa Amani wa Ulaya (EPF), ambao hadi sasa umewezesha utoaji wa euro bilioni 3.1 kutoka kote Ulaya; fedha hizi zitapatikana kati ya 2022 na 2026, kusaidia utoaji wa vifaa vya kijeshi kutoka EU.

Mwezi wa nne mwaka huu Marekani ilitangaza kuitumia  Ukraine silaha huku kukiwa na udhibiti wa utumiaji wa silaha hizo huku  wachambuzi wakihoji  kuwa  Marekani inafanya hivyo ikijaribu kuepuka mvutano na Urusi.

Mwezi Januari mwanasiasa mmoja nchini humo alisema kutokana na kanuni za usafirishaji, Marekani ina nia ya  kuondoa madini ya Urani katika vifaru hivyo vya Abrams kabla ya kuvituma Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.